THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

KAMATI YA BUNGE YA VIWANDA, BIASHARA NA MAZINGIRA YATEMBELEA CHANZO CHA MAJI, IFUNDA

Kamati ya Kudumu ya Bunge Biashara na Mazingira mwishoni mwa wiki imetembea chanzo cha Maji ‘Mkaa’ kilichopo Tarafa ya Kiponzelo, Kata ya Ifunda, Mkoani Iringa.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Innocent Bashungwa ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Iringa kwa jitihada zao za kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya kunyweshea mifugo ili kuendelea kulinda vyanzo vya maji na kuwataka kuondoa miti iliyopo pembezoni mwa chanzo hicho ambayo inanyonya maji kwa wingi.

Kwa upande mwingine, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Kangi Lugola amezitaka Halmashauri na Wilaya zote nchini kupanda miti kwa wingi ambayo ni rafiki kwa mazingira. “Endapo tutapanda miti kwa wingi, tutaendelea kuwa na mvua za kutosha na kila Halmshauri zinatakiwa kuwa na Sheria ndogo ndogo za Mazingira”.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza amewataka waheshiwa wabunge kuwa mstari wa mbele kuhimiza kilimo cha umwagiliaji kwa kutimia ‘matone’ ili kupunguza matumizi ya maji katika maeneo yao.
Diwani wa Kata ya Ifunda Bw. Elicus Chumila Ngwetta akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira mara baada ya kutembelea eneo la Ifunda na kujionea chanzo cha maji ‘Mkaa’ kilichohifadhiwa vizuri. Uhifadhi wa vyanzo vya maji ni muhimu sana kwa mustakabali wa nchi yetu. Kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Kangi Lugola.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Kangi Lugola akifafanua jambo mbele ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira. Kamati ya Bunge mwishoni mwa wiki ilipata fursa ya kutembelea chanzo cha maji ‘Mkaa’ kilichopo Tarafa ya Kiponzelo, Kata ya Ifunda, Mkoa wa Iringa.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Kangi Lugola akisisitiza jambo mbele ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira mara baada ya kutembelea chanzo cha maji ‘Mkaa’ kinachopeleka maji yake Mto Lyandembela ambao nao unamwaga maji Ruaha Mkuu mwaka mzima, Mto ambao ni muhimu sana kwa ustawi wa viumbe hai. Kushoto ni Mhe. Hawa Mwaifunga na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Innocent Bashungwa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza akiwaonyesha waheshimiwa wabunge wa Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira eneo maalumu lililotengwa kwa ajili ya mifugo kunywa maji katika eneo la Ifunda ikiwa ni jitahada za Mkoa huo kuhifadhi vyanzo vya maji.