Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

Kesi dhidi ya Mhasibu  Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Godfrey Gugai anayedaiwa kuwa na  utajiri wa kutisha kwa kumiliki mali zenye thamani ya Sh. 3 bilioni ambazo haziendani na kipato chake kuanza kusikilizwa mapema mwezi ujao.

Hayo yameelezwa leo Machi 20, 2018 na wakili wa serikali kutoka Takukuru, Vitalis Peter mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba. 

"Mheshimiwa kesi hii leo ilikuja kwa ajili ya kutajwa lakini upelelezi umekamilika, tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuja kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali (PH).

Kufuatia taarifa hiyo, hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Aprili 10, mwaka huu. Kwa ajili ya washtakiwa kusomewa Maelezo ya awali.

Mbali na Gugai, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasini Katera

Washtakiwa hao wanaokabiliwa na mashtaka 43 yakiwemo 20 ya utakatishaji fedha haramu, kumiliki mali zisizoendana na kipato na kughushi mikataba ya mauziano ya viwanja katika maeneo mbalimbali.

Gugai na wenzake wanasota mahabusu kutokana na kukabiliwa na mashtaka ya utakatishaji fedha ambayo hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...