Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

BARAZA la Madiwani wa Jiji la  Dar es Salaam limeomba kufahamu kiasi cha fedha kinachopatikana katika Soko la Kariakoo maana wamechoshwa na kauli ya kwamba soko hilo linaendeshwa kwa hasara.

Baadhi ya madiwani hao wamekiambia kikao cha Baraza la Madiwani wa Jiji hilo leo jijini Dar es Salaam wamesema Jiji linamiliki soko kwa asilimia 51.Diwani wa Kata ya Mbezi Humphrey Sambo amekiomba kikao hicho kupata taarifa za mapato ya soko hilo kwani kwa mtazamo wa kawaida wamedai fedha inayopatikana ni nyingi lakini wao wanaambiwa linaendeshwa kwa hasara.

"Tufuatilie ili kujua nini ambacho kinaendelea katika Soko la Kariakoo kwani nimechoka kusikia kila siku wanapata hasara lakini watu wanakwenda kazini," amesema.Amefafanua kwa kuwa Jiji linahisa ya asilimia 51 ni vema ikajulikana kinachopatikana na mgao wa Jiji ni kiasi gani.

Kwa upande wa Diwani wa Kata ya Tabata Patrick Asenga amesema soko la Kariakoo si kweli linapata hasara kwani hata vizimba vya biashara vilivyopo kodi yake ni Sh.300,000 hadi Sh.400,000.Amesema ni vema Jiji likatoa kauli ya kuwaita wanaosimamia soko hilo ili waeleze kuhusu soko hilo na kwamba hakubaliani na kauli ya soko kuendeshwa kwa hasara.

Kutokana na maelezo hayo ya madiwani,Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amemuomba Mkurugenzi wa Jiji hilo kuyafanyia kazi na kwenye kikao kijacho majibu yatolewe."Mkurugenzi wa Jiji naomba ukae na menejimenti yao  kushughulikia suala hili kwanza na  na menejimenti yake na baada ya hapo taarifa itolewe," amesema.
Mstahki Meya wa jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita akiongoza kikao cha robo ya pili ya baraza la madiwani leo, kushoto ni Mkurugenzi wa jiji Sipora Liana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...