Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma akifungua kikao cha  Majaji wa Mahakama ya Rufani, lengo la kikao hicho cha siku moja kimelenga katika kufanya tathmini yaUtendaji kazi wa Mahakama ya Rufani kwa mwaka 2017 na kuweka Mkakati na malengo ya mwaka, 2018, kulia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani (T),. Benard Luanda. 
Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Katarina Revokati akitoa Mada ya Mpango Mkakati wa Mahakama kwa Majaji wa Mahakama ya Rufani waliopo katika kikao cha tathmini na uwekaji wa mpango wa malengo ya utekelezaji kwa mwaka huu.
Msajili-Mahakama ya Rufani (T) akitoa Mada katika Kikao cha Wahe. Majaji wa Mahakama ya Rufani (T), katika Mada yake Mhe. Msajili amesema kuwa Mahakama ya Rufani imefanikiwa kushusha kiwango cha mlundikano kutoka asilimia 37 mwaka 2016 hadi asilimia 10 mwishoni mwa Desemba, 2017.
Baadhi ya Majaji wa Mahakama ya Rufani wakiwa katika hicho kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya ‘Oceanic’ iliyopo Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
 Jaji Mkuu,  Majaji wa Mahakama ya Rufani, Wasajili wa Mahakama ya Rufani na Wasaidizi wa Sheria wa Majaji wa Mahakama ya Rufani wakiwa kwenye picha ya pamoja.
(Picha na Mary Gwera)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...