Na Bashir Yakub.

Inaweza kuwa nyaraka muhimu kama hati ya nyumba, mkataba wa mauziano au mkataba mwingine wowote, wosia, kadi ya gari au ya mashine yoyote,hati ya kusimamia mirathi, cheti cha ndoa au vyeti vinginevyo, na nyaraka nyingine mbalimbali.

Nyaraka hii inaweza kuwa inatakiwa sehemu muhimu kama mahakamani ili kuthibitisha shauri au kesi yako. Na inaweza ikawa ni nyaraka ambayo kuwepo kwake ndio kushinda kwako na kutokuwepo kwake ndio kushindwa kwako.

Pamoja na umuhimu wa nyaraka hii bado umeitafuta kote pa kutafuta na hukuweza kuipata. Au hukuitafuta madhali tu unajua ilishapotea au iko mikononi mwa mtu ambaye hujui alipo na hawezi kupatikana. Katika mazingira ya namna hiyo makala yataeleza vitu vichache vinavyoweza kusaidia kutoka Sura ya sita,Sheria ya Ushahidi.

1. USHAHIDI WAKO.

Kitu kikubwa kinachomsaidia mtu kushinda kesi mahakamani ni ushahidi. Kadhalika kushindwa kwako pia ni ushahidi. Ukisema hiki kiwanja au nyumba ni yangu unatakiwa kuonesha hati au mkataba wa mauziano au vyote viwili.

Ukisema hili gari ni langu kadhalika uoneshe kadi yenye jina lako ama vinginevyo. Ukisema nilikuwa na ndoa halali uoneshe cheti cha ndoa ama vinginevyo. Ukisema nilimuuzia au kununua kitu fulani uoneshe mkataba ama risiti,vivyo hivyo nk, nk.

Hakimu au Jaji si mtu ambaye anakuwa eneo la tukio na hivyo kuwa katika nafasi ya kujua nini kilitokea huko. Yeye hajui chochote kilichotokea na hivyo taarifa zote anazipata kwenu mnaoshitakiana. Kwa msingi huu yupo katika wakati mgumu kuamua nani yuko sahihi na nani hayuko sahihi kwa kitu ambacho hakushuhudia na hakijui.

Kama hivi ndivyo kitu pekee cha kumuongoza hakimu/jaji huyu ambaye hakuwepo wakati mnadhulumiana, ni ushahidi wa kila mmoja atakaowasilisha. Hataangalia suraya mtu, kulia machozi kwa mtu, kuongea kwa kujiamini au kwa unyonge kwa mtu, umri wa mtu, rangi ya mtu,wala jinsia, bali ushahidi ulio uliowasilishwa na mtu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...