Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo ameanza ziara ya siku tatu Pemba ikiwa na lengo la kuhamasisha shughuli za maendeleo. 
Makamu wa Rais ambaye amewasili Pemba alasiri ya leo na kupokelewa na viongozi mbali mbali wa Serikali na Chama ambapo alipokea taarifa za mikoa miwili ya Pemba. Pia Makamu wa Rais alizuru kaburi la Dkt. Omar Ali Juma lililopo Wawi, Pemba na kuweka shada la maua. 
Aidha Makamu wa Rais aliwataka Wananchi wa Chumbageni kukumbuka historia na kurudi nyumbani, Makamu wa Rais aliyasema hayo mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Tawi la CCM Chumbageni Wambaa. 
Kesho Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anatazamiwa kuendelea na ziara yake ambapo ataweka jiwe la msingi katika Kituo cha Huduma za Mama na Mtoto Shumba Vyamboni .
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikabidhiwa shada la maua kwenye kaburi la Marehemu Dkt. Omar Ali Juma lililopo Wawi,Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua kwenye kaburi la Marehemu Dkt. Omar Ali Juma lililopo Wawi,Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)Dk Omar Ali Juma (26 Juni 1941 – 4 Julai 2001) alikuwa Makamu wa Rais wa Serikali ya Awamu ya Tatu nchini Tanzania, iliyokuwa inaongozwa na Rais Benjamin William Mkapa


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...