Na Emmanuel Masaka, Globu ya jamii

MAMA mwenye mtoto mwenye nguvu za ajabu anayeishi Mtaa wa Kwa Mbela uliopo Mburahati Mianzini Salama Omar amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kumsaidia katika matibabu ya mwanaye.

Mbali ya kumuomba Makonda kumsaidia matiabu ya mtoto wake Mzamiry Said(7), pia ametumia nafasi hiyo kuelezea namna ambavyo mumewe aliyefunga naye ndoa mwaka 2009 alivyomtekeleza yeye na mtoto.

Akizungumza na Michuzi blog leo jijini Dar es Salaam Salama amesema anaishi maisha yenye changamoto nyingi anakabiliana nazo katika malezi ya mtoto wake ambaye ameeleza amekwenda kwenye hospitali mbalimbali ikiwemo Hospitali ya Taifa  Muhimbili na CCBRT.

Amefafanua na kote huko alikokwenda madaktari wamechukua vipimo vyote vikiwemo vya kuangalia iwapo ana tatizo la akili au ulemavu lakini wamemthibitisha matatizo hayo ila anakumbuka mmoja wa madaktari wa Muhimbili anayeshughulikia watu wenye magonjwa ya akili anakumbuka alimwambia mwanaye hata pona , hivyo ataendelea kuwa hivyo katika maisha yake yote.

"Ni kweli mwanagu sasa ana maiaka saba na tatizo bado lipo.Ana nguvu nyingi na anapocheza na wenzake unakuwa makini kufuatilia maana anaweza kufanya chochote ambacho si kizuri. Napata shida kwenye malezi ya mwanangu tangu alipozalizwa.

Nimejitahidi katika matibabu lakini hali iko vile vile.Muda wote inabidi niwe namchunga asiende mbali kwani unaweza kumuacha akaenda kucheza na watoto wengine mtaani lakini kutokana na nguvu alizonazo anaweza hata kujeruhi.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...