Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii.

Taasisi ya Young Scientist Tanzania (YST) inapenda kuwaalika wanafunzi wa shule za sekondari pamoja na walimu kushiriki katika maonesho ya YST 2018 yatakayofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) kuanzia tarehe 1 hadi 2 Agosti mwaka huu.

Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mwanzilishi mwenza wa taasisi ya YST Gosbert Kamugisha ameeleza kuwa Wanafunzi wanaombwa kutuma kazi mradi zao za kiutafiti wa kisayansi kwa YST hadi  tarehe 21 Aprili, wanafunzi 200 watachaguliwa na kuonesha tafiti zao za ugunduzi wa kisayansi na kupewa mafunzo ya ziada ya kuendeleza tafiti zao toka kwa wataalamu wabobevu kutoka YST.

Nyanja mbalimbali zitaangaliwa na watafiti chipukizi hao katika sayansi kama vile katika Kemia, Fizikia, Hisabati, Bailojia, na Ecolojia na kazi hizo zitalenga katika kuleta masuluhisho katika masuala ya afya, kilimo, chakula, mawasiliano, elimu, usafiri na mabadiliko ya tabia nchi.

Zawadi mbalimbali zitatolewa kwa washiriki watakaofanya vizuri kama fedha, medali pamoja na udhamini wa masomo ya elimu ya juu kwa wanafunzi watakaofanya vizuri.

Taasisi ya YST inaomba ushirikiano kwa wazazi, walimu, Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO'S) kushirikiana nao ili kuweza kupata masuluhisho ya kijamii na uchumi yanayoikumba jamii kwa sasa kupitia wanafunzi wetu(wanasayansi chipukizi.)
Mwanzilishi wa Taasisi ya Young Scientist Tanzania (YST),Joseph C lowry akizungunmza na waanshi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu  washiriki watakaofanya vizuri kama fedha, medali pamoja na udhamini wa masomo ya elimu ya juu kwa wanafunzi watakaofanya vizuri.(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii).
 Mwazilishi Mweza wa Taasisi ya YST,Gosbert  Kamugisha akizungumza na waandishi wa habari hawapo pihani juu ya maonesho ya YST 2018 yatakayofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) kuanzia tarehe 1 hadi 2 Agosti mwaka huu.
 Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Mwanzilishi mwenza  wa Taasisi ya YST,Gosbert  Kamugisha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...