Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, akimuongoza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, kukagua mazingira ya ndani ya moja kati ya Vituo vya Polisi Vinavyohamishika baada ya kuzinduliwa mwishoni mwa wiki na naibu waziri huyo lengo ikiwa ni kusogeza huduma za kipolisi karibu na wananchi.Uzinduzi huo ulifanyika katika Viwanja vya Polisi Oysterbay,jijini Dar es Salaam.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Polisi Jamii Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Ahmada Khamis(kulia), baada ya kuzindua Vituo vya Polisi Vinavyohamishika katika Viwanja vya Polisi Oysterbay, lengo ikiwa ni usogezaji karibu wa huduma za kipolisi kwa wananchi.Katikati ni Mkuu wa Shirika linaloshughulika na Usafirishaji wa Wakimbizi nchini (IOM), Dk. Qasim Sufi.Tukio hilo limefanyika mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akijibu maswali ya Waandishi wa Habari baada ya Uzinduzi wa Vituo vya Polisi Vinavyohamishika lengo ikiwa ni usogezaji wa huduma za kipolisi kwa wananchi.Tukio hilo limefanyika mwishoni mwa wiki katika Viwanja vya Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ,Mhandisi Hamad Masauni, akiwasili katika Viwanja vya Polisi Oysterbay wakati wa Uzinduzi wa Vituo vya Polisi Vinavyohamishika lengo ikiwa ni kusogeza huduma za kipolisi karibu na wananchi.Kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa na wengine kutoka kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Salum Hamduni, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke, Emmanuel Lukula na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Jumanne Muliro.Tukio hilo limefanyika mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wanne kulia), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Jeshi la Polisi na wageni waalikwa baada ya kuzindua Vituo vya Polisi Vinavyohamishika, lengo ikiwa ni kusogeza huduma za kipolisi kwa wananchi. Waliosimama ni Kikundi cha Polisi Jamii cha Mkoa wa Kipolisi Kinondoni.Tukio hilo limefanyika mwishoni mwa wiki katika Viwanja vya Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...