THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

MAYANGA AITA 23 TAIFA STARS KUWAKABILI ALGERIA NA DR CONGO

Kikosi cha wachezaji 23 wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars kitakachocheza michezo miwili ya kirafiki kwenye tarehe za kalenda ya FIFA dhidi ya Algeria na DR Congo kimetajwa leo Alhamis Machi 8, 2018.

Kikosi hicho kitaingia kambini Machi 18, 2018 kwenye hotel ya SeaScape na kuondoka Machi 19, 2018 kuelekea Algeria kwa mchezo utakaochezwa Machi 22, 2018 kitarudi Tanzania Machi 24, 2018 kujiandaa na mchezo wa pili utakaochezwa Uwanja wa Taifa Machi 27, 2018 na DR Congo.

Kikosi kilichoitwa: 
WALINDA MLANGO.
  1.Aishi Manula  (Simba),   2.Ramadhani Kabwili  (Young Africans)
  3.Abdulrahman Mohamed (JKU)
  
WALINZI WA PEMBENI.
  4.Shomari Kapombe (Simba),  5.Hasan Kesy (Young Africans)
  6.Gadiel Michael(Young Africans)
  
WALINZI WA KATI.
  7.Kelvin Yondan(Young Africans),   8.Abdi Banda (Baroka)
  9.Erasto Nyoni(Simba)

VIUNGO WA KATI .
  10.Hamisi Abdallah  (AFC Leopards),   11.Mudathir Yahaya (Singida United),   12.Said Ndemla  (Simba),   13.Faisal Salum (JKU),   14.Abdulazizi Makame (Taifa Jang’ombe)

VIUNGO WA PEMBENI.
  15.Farid Mussa ( Teneriffe),   16.Thomas Ulimwengu  (FK Sloboda Tuzla)
  17.Ibrahim Ajib  (Young Africans),   18.Shiza kichuya  (Simba),  19.Mohamed Issa  (Mtibwa)

WASHAMBULIAJI.
  20.Mbwana Samata (KRC Genk),   21.Saimon Msuva (El Jadida),   22.John Bocco  (Simba),   23.Zayd Yahaya (Azam FC)

BENCHI LA UFUNDI.
  1.Salum Mayanga,   2.Hemed Morocco,   3.Patrick Mwangata,   4.Dani Msangi,   5.Dr.Yomba,   6.Dr.Gilbart Kigadya na   7.Ally Ruvu