Na Dotto Mwaibale, Chalinze

WAKULIMA wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Mkoani wa Pwani wamefurahia kupokea mbegu bora ya mahindi aina ya Wema 2109 kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa na Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB) kwa ajili ya kupandwa kwenye mashamba darasa katika halmashauri hiyo.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya mbegu hiyo kwenye uzinduzi wa mashamba darasa katika vijiji vya Diozile na Kibindu vilivyopo Kata ya Msoga mkoani humo Ofisa Kilimo wa Mkoa wa Pwani,Kapilima George alisema mbegu hiyo itasaidia kuongeza tija ya uzalishaji wa mahindi katika halmshauri hiyo hivyo amewataka wakulima kuichangamkia.

"Tuwashukuru COSTECH na OFAB kwa kutuletea mbegu hii ambayo kwetu itakuwa ni mkombozi mkubwa katika mkoa wetu hasa kwa wakulima wa Kata ya Kibindu ambao ni vinara kwa kilimo cha mahindi katika mkoa wetu" alisema George.

Alisema mkoa wa Pwani kwa mwaka jana ulizalisha tani 110 za mahindi huku tani 65 zikizalishwa na Kata ya Kibindu jambo la kuwapongeza wakulima wa kata hiyo.Alisema mbegu hiyo itaongeza msukumo wa kilimo ilimo cha mahindi kwenye halmashauri hiyo hivyo kujikwamua kupata baa la njaa na ziada kuuza.

Mkurugenzi wa Fedha wa Fedha na Utawala wa COSTECH, Shabani Hussein (wa pili kulia), akimkabidhi Mwenyekiti wa Kikundi cha Gezaulole, Ali Hussein Rajab (kulia), mbegu ya mahindi ya Wema 2109 katika uzinduzi wa shamba darasa uliofanyika leo katika Kata ya Msoga mkoani Pwani. Wengine kutoka kushoto ni Ofisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Jovin Bararata, Matifiti Kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga mkoani Morogoro, Mikidadi Hamidu, na Ofisa Kilimo Mkoa wa Pwani Kapilima George. Mbegu hiyo imetolewa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa na Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB). 
Mkulima wa kutoka Kikundi cha Gezaulole kilichopo Msoga, Shabani Mbogo akielezea changamoto za kilimo katika eneo hilo.

Ofisa Kilimo wa Mkoa wa Pwani,Kapilima George (wa pili kulia), akizungumza wakati wa uzinduzi wa shamba darasa la Kikundi cha Gezaulole katika Kata ya Msoga. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...