Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MEYA wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amezitaka halmashauri zote katika jiji hilp kuajiri watumishi ambao watakuwa wanazika miili ya watu ambao watabainika kutokuwa na ndugu wa kuwazika.

Ametoa kauli hiyo leo kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam ,ambapo amewaambia madiwani hao kuna taarifa amezipata za halmashauri kutokuajiri watumishi kwa akili ya kuzika watu wasiokuwa na ndugu.

Mwita amesema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam pamoja na halmashauri nyingine zilizopo jijini humo walikubaliana kuzika watu wasiokuwa na ndugu Dar."Hivyo marehemu wanapokuwa wamekaa muda mrefu wanalazimika kuzika na Jijijiji,na tulikubali kuchangia usafiri,dawa na sanda," amesema.

Amefafanua kuwa watu hao wasiokuwa na ndugu wanapokufa wapo ambao wanakaa hospitalini zaidi ya siku 20,hivyo wapo ambao wanazika kwenye halmashauri mbalimbali.Hivyo wakati Jiji la Dar es Salaam likitimiza wajibu katika kupumzisha mwili wa marehemu,halmashauro jukumu lao ni kutoa watumishi kwa ajili ya kuzika.

Amefafanua taarifa alizonazo ni Halmashauri ya Kinondoni pekee ndio ambayo imeajiri watumishi kwa ajili ua kuzika miili ya watu ambao wamefariko na hawana ndugu.Hivyo amezikumbusha halmashauri zote kuajiri watumishi hao ili kufanikisha kupumzisha miili hiyo.

"Ni wajibu wa halmashauri kuhakikisha wanafanikisha kupatikana kwa watumishi hao haraka," amesema Meya Mwita.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...