Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA)imeamua kuzifutia leseni za kampuni nne za ushauri na udalali wa bima (Insurance Brokers).

Akizungumza leo Dar es Salaam, Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Kamishna Dk.Baghayo Saqware amesema kampuni hizo za udalali na ushauri wa Bima yaliyofungiwa yalikuwa yamesajiliwa na kupewa leseni ya kufanya biashara ya bima kwa mujibu wa sheria ya Bima namba 10 ya mwaka 2009.

Ametaja kampuni ambazo zimefutiwa leseni ya udalali wa bima ni kampuni ya udalali wa Bima ya HANS, ENDEAVOUR, LEGEND OF EAST AFRICA, pamoja na SWIFT.

Kamishna Dk.Saqware ameongeza kapuni hizo zimefungiwa kwa kosa la kutowasilisha ada za bima kwa kampuni ya bima ambapo mawakili wa kampuni wamefunga ofisi bila kulipa ada stahiki na kufuta taratibu zilizowekwa za kufunga ofisi.

Aidha amesema mamlaka imetathimini mwenendo wa kampuni hizo na kuona ni vema ikachukua hatua za haraka zilizo ndani ya uwezo wake kwa mujibu wa sheria ya Bima Na.10 ya mwaka 2009 kifungu cha 74, ambayo ni kuyafutia leseni ya biashara kampuni hizo.

Dk.Baghayo amesema kinachotakuwa ni kuhakikisha wateja wa Bima kupata haki na heshima ya soko hilo inalindwa hata baada ya kampuni hizo kufutiwa leseni.

Amewataka wananchi kutambua uwepo wa mamlaka ya usimamizi wa shghuli za Bima hapa Nchini."

Wananchi wasilalamike na kunung’unika pale wanapopata matatizo ya kibima na kwa kutokuja wapi pa kwenda.

Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Kamishna Dk.Baghayo Saqware akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es Salaam wakati akitangaza agizo la kuzifutia leseni za makampuni manne ya Ushauri na Udalali wa bima (Insurance Brokers) kwa kukiuka malengo ya leseni zao. Picha na Cathbert Kajuna.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...