Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo amesema kuwa jumla ya viwanda 1,285 kati ya 2,600 vimejengwa katika mikoa mbalimbali ikiwa ni miezi mitatu tangu atoe agizo la ujenzi wa viwanda 100 kwa kila mkoa.

Akizungumza katika kikao kazi cha kupitia bajeti ya TAMISEMI na Mikoa, kilichofanyika leo mjini Dodoma Jafo amesema viwanda hivyo vilivyojengwa ni sawa na asilimia 49.4 na kutoa ajira.Amesema agizo hilo bado linaendelea kutekelezwa ambapo hadi kufikia Desemba 31, mwaka huu kila mkoa unatakiwa kuwa na viwanda 100 ambavyo ni sawa na viwanda 2600.

Amebainisha kuwa kupitia wakuu wa mikoa ajenda ya Rais John Magufuli ya Viwanda inatekelezwa na kuwataka waendelee kuitekeleza.Kwa mujibu wa Waziri Jafo, viwanda vidogo vinavyojengwa  ni vile vinavyoanzia sh.milioni 2.5 hadi sh.milioni 10.

Akizungumzia kuhusu maandalizi ya bajeti kwa mwaka huu Waziri Jafo amewataka Makatibu Tawala wa Mikoa kuhakikisha kuwa wanawapitisha vizuri Wakuu wa Mikoa ili waelewe bajeti za mikoa yao na wahakikishe kuwa randama zinakaa vizuri.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo akifunga kikao kazi kilichohusisha Wakuu wa Mikoa,Makatibu Tawala wa mikoa na Wakurugenzi wa Idara Tamisemi leo mjini Dodoma.
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo akifunga kikao kazi kilichohusisha Wakuu wa Mikoa,Makatibu Tawala wa mikoa na Wakurugenzi wa Idara Tamisemi leo mjini Dodoma.
 Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya, Ofisi ya Rais, Tamisemi,Dk.Zainabu Chaula akizungumza wakati wa kikao kazi cha Ofisi hiyo kilichojumuisha Wakuu wa Mikoa,Katibu Tawala wa mikoa,Wakuu wa Idara Ofisi ya Tamisemi kilichofanyika leo mjini Dodoma.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akitoa taarifa ya Mkoa wake kuhusu utekelezaji wa agizo la ujenzi wa viwanda 100 kwenye kikao kazi cha Wakuu wa Mikoa,Makatibu Tawala wa mikoa, kilichofanyika Wakurugenzi wa Idara Tamisemi leo mjini Dodoma.
 Baadhi ya Wakuu wa Mikoa wakishiriki kikao kazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...