Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM Mkoa wa Pwani,Ramadhani Mlao,akizungumza na wajumbe wa baraza la UVCCM wa Wilaya ya Mafia kuhusu kupeleka sehemu husika mgogoro wa wananchi na hifadhi ya bahari pamoja na kuwahimiza wanakipigania chama kishinde uchaguzi ujaowa serikali za mitaa. Kushoto ni Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani,Charangwa Makwiro na Mwenyekiti wa UVCCM wa Wilaya ya Mafia,Amina Tuki.Picha Zote na Elisa Shunda.
Wajumbe wa Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Mafia wakifuatilia kwa makini mkutano huo.

NA ELISA SHUNDA,MAFIA.
MJUMBE wa Baraza Kuu la Taifa Mkoa wa Pwani,Ramdhan Mlao amewahakikishia vijana wa Wilaya ya Mafia (Kisiwa) kulifanyia kazi suala la mgogoro uliopo katika ya hifadhi ya bahari na wananchi wanaoishi katika wilaya hiyo ambayo inajumuisha na visiwa vidogo vya Chole,Jibondo na Juani (Visiwa vidogo) kwa kulifikisha jambo hilo kwa viongozi wanaouhusika.

Mlao ametoa kauli hiyo leo wakati anajibu swali lililoulizwa na Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tawi la Chole,Khamisi Musa ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Umoja wa Vijana CCM wilaya hiyo aliyeuliza kuhusu mgogoro wa wananchi hao kuzuiliwa kufanya shughuli za uvuvi wa samaki kwa kuwa maeneo hayo kwa sasa yamechaguliwa kuwa hifadhi za bahari kulingana na samaki aina ya Papa waliopo katika maeneo hayo.

Hivyo amesema ameyapokea malalamiko yao na kuahidi kulifikisha jambo hilo katika sehemu husika ili kusaidia vijana,wananchi hata chama chake cha CCM.

“Kwa historia tuliyoipata pamoja na nyie kutueleza hapa hili tatizo lina muda kidogo lakini pia  kuna athari kubwa kwa watu wa Mafia na pia litatuathiri sisi CCM kama hatutalifanyia ufumbuzi yakinifu ili watu hawa waweze kuishi salama katika maeneo yao upo mgogoro mkubwa baina ya hifadhi ya bahari na wananchi.

"Mgogoro huu kimsingi kama isipopazika sauti kwa viongozi kwa mustakabali mema kwa mujibu wa watu wa Mafia basi kisiwa hiki hakitakuwa salama, wenzetu hawa wa hifadhi ya bahari wanaonekana tatizo lakini suluhu si kulikimbia tatizo suluhu ni kukaa pamoja wao na nyie mnahitajiana watu wa hifadhi wanawahitaji na nyie mnawahitaji pia kwa kuwa nyie ndiyo wenye mafia yenu lakini katika bahari hii ushuru unapatikana hivyo tatizo hili ni lazima lisuluhishwe mapema” amesema Mlao.

Mbaraza Mlao amesema atayapeleka changamoto hizo kwa Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo Abdallah Ulega ambaye pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani ni msikivu na mchapakazi akaongeza kuwa atampelekea msisitizo kuona picha ya ukubwa wa tatizo hili kwa kuwa kati ya wahusika wa jambo hili yeye na wizara hii ni wahusika muhimu katika kulitatua mgogoro huu.

Aidha Mbaraza Mlao ameongeza kwa kueleza watahakikisha jambo hilo linapata ufumbuzi kwa kuwa kama mgogoro huo usipofanyiwa kazi vijana hao watapata shida kukinadi Chama Cha Mapinduzi wakati wa uchaguzi suluhisho ni kulifanyia ufumbuzi suala hilo kwa kuwa kama wasipolitatua jambo hilo itafika wakati wananchi watawauliza kama mmeshindwa kututatulia mgogoro huu wa hifadhi za bahari tutawaamini vipi wakati jambo hili mmeshindwa kututetea.

“Lengo la dhamira yetu ni kusaidiana na kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani na usalama katika maeneo yao hatuwakatai ndugu zetu wa hifadhi za bahari  lakini tunataka kwenye maisha haya kila mmoja aishi kwenye eneo lake akiwa salama salmini na afurahie maisha ya uishi wa Utanzania wake tumelipokea jambo hili tunalifanyia kazi ndugu viongozi mtapata majibu juu ya jambo hili,"amesema Mlao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...