THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

MSAJILI AZITAKA NGOs KUWASILISHA TAARIFA

MASHIRIKA yasiyo ya Kiserikali nchini (NGOs) yaaswa kuwasilisha taarifa za Mwaka kwa mujibu wa Kifungu Na. 29 cha Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 na Kanuni Na. 10 ya Kanuni za Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2004 (GN 152, 2004) kabla ya tarehe 15 Aprili, 2018.

Hayo yameainishwa katika taarifa ya Msajili wa Mashirika yasiyo ya kiserikali Marcel Katemba kwa vyombo vya habari  jijini Dar es Salaam leo. Taarifa hiyo inaeleza kuwa “Mashirika yasiyo ya kiserikali kuwasilisha Taarifa za Mwaka kwa mujibu wa Kifungu Na. 29 cha Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya mwaka 2002 na Kanuni Na. 10 ya Kanuni za Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2004 (GN 152, 2004), kama ilivyorekebishwa na Kanuni Na. 6 ya Kanuni za Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2014 (GN 8, 2015)”.

 “Taarifa hiyo ijumuishe Taarifa za utendaji kazi, Taarifa za fedha zilizokaguliwa, NGO Fomu Na.10 na Stakabadhi ya malipo ya ada ya mwaka” 

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Mashirika yatakayoshindwa kutekeleza agizo hili ndani ya kipindi tajwa, yatachukuliwa hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kutozwa faini.