Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imepokea msaada wa vitanda 14, magodoro 12  pamoja na drip stands kutoka Australia Tanzania Society ambavyo vitasaida kuimarisha utoaji wa huduma hospitalini  hapo.

Akipokea msada huo jijini Dar es Salaam  kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Dkt.  Juliethi Magandi amesema kwa muda mrefu hospitali imekua na ushirikiano na tasisi hiyo katika masuala mbalimbali ikiwemo kufanya  upasuaji wa ubingwa wa juu.

“Kipekee nichukue fursa hii kuwashukuru rafiki zetu hawa Australia Tanzania Society kwa msaada huu  walioutoa kwani tumekua tukishirikiana kwa zaidi ya miaka mitatu sasa,”.  amesema Dkt. Magandi.

Amesema Hospitali ya Taifa Muhimbili ina jumla ya vitanda 1,507 na kwamba kina mama wajawazito na watoto pekee wanatumia karibu  ya nusu ya vitanda hivyo.  “Hivyo  msaada huo umekuja wakati muafaka  kwani hospitali bado ina mahitaji kutokana na kutoa huduma zake kila siku kwa saa 24,”.
 Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Julieth Magandi akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kabla kukabidhiwa vitanda 14 na magodoro 12 ambayo yametolewa na Australia Tanzania Society. Kulia ni Mkurugenzi wa Australia Tanzania Society, James Chialo na kushoto ni Mkuu wa Idara ya Uuguzi na Mazingira Muhimbili, Zuhura Mawona.
 Muuguzi Alice Msonda na Velena Joahackim wakitandika kitanda baada ya kukabidhiwa vitanda na magodoro na Australia Tanzania Society.
 Mkurugenzi wa Australia Tanzania Society, James Chialo akimkabidhi Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa Muhimbili, Dkt. Julieth Magandi vitanda 14 leo. Katikati ni Mkuu wa Idara ya Uuguzi na Mazingira Muhimbili, Zuhura Mawona.
Mkurugenzi wa Australia Tanzania Society, James Chialo akizungumza na waandishi wa habari leo kabla ya kukabidhi vitanda hivyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...