Mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo katika eneo la Nyahua wilayani Uyui Mkoani Tabora imesababisha kukatika kwa barabara kuu ya Tabora kupitia Itigi hadi Dodoma na kusababisha magari ya abiria na mizigo kwishindwa kuendelea na safari zake kwa kutumia barabara hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika eneo la tukio Meneja wa Wakala wa Barabara )TANROADS) Mkoa wa Tabora  Mhandisi Damian Ndabalinze alisema mvua zilizonyesha katika maeneo hayo zimesababisha kukatika kwa eneo hilo ambapo ndipo barabara ya lami inaishia.

Aliwataka madereva wa magari ya aina yoyote kudiriki kupita katika aina hilo kwa sababu wanaweza kuhatarisha maisha yao na abiria na mizigo.

Ndabalinze alisema dereva yoyote atakayekaidi na kuamua kupita katika eneo hilo kwa kulazimisha jambo lolote litakalompata itakuwa ni yeye kajisababishia na asilelekeze lawama kwa chombo chochote.
  Baadhi ya wasafiri na wakazi wa Nyahua wilayani Uyui wakiwa katika eneo ambalo barabara imekatika kutoka na mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha kukatika kwa mawasiliano baina ya Itigi na Tabora. Nyuma ni basi dogo la Prince  Ramigo linalofanya safari zake kutoka Tabora kwenda Dodoma kupitia Itigi.
Baadhi ya wasafiri kutoka katika Basi la Prince Ramigo na wakazi wa Nyahua wilayani Uyui wakijaribu kuvuka jana katika eneo ambalo barabara imekatika kutoka na mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha kukatika kwa mawasiliano baina ya Itigi na Tabora. Nyuma ni basi dogo la Prince  Ramigo linalofanya safari zake kutoka Tabora kwenda Dodoma kupitia Itigi. 
  Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Tabora,  Mhandisi Damian Ndabalinze akizungumza na waandishi wa habari na wasafiri jana mara baada ya kutembelea eneo la tukio ili kujionea uharibifu wa barabara ulitokana na mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha kukatika kwa mawasiliano baina ya Itigi na Tabora
 Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoani Tabora SP Emilian  Kamuhanda akizungumza na waandishi wa habari na wasafiri jana mara baada ya kutembelea eneo la tukio ili kujionea uharibifu wa barabara ulitokana na mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha kukatika kwa mawasiliano baina ya Itigi na Tabora na kisha kutoa tahadhari kwa Madereva kutodiriki kupita katika eneo hilo.
  Basi la Prince Ramigo linalosafirisha abiria kutoka Dodoma kwenda Tabora likiwa limekwamwa katikati ya maji jana mara baada ya Dereva kujaribu kupita. Picha na Tiganya Vincent

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...