Na Elisa Shunda, Kibiti
MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Makwiro amewataka vijana wa mkoa huo kutojihusisha na mambo ambayo hayana tija kwa Taifa huku pia akipokea wanachama wapya 60 ambao wameamua kujiuna na umoja huo mkoani Pwani.

Wanachama hao wamejiunga leo wakati wa ziara yake ambayo aliongoza na wajumbe wa baraza kuu la UVCCM Mkoa wa Pwani  wakati anazungmza na wajumbe wa baraza la wilayani Kibiti.

Akizungumza baada ya kuwapokea vijana hao, Mwenyekiti Charangwa Makwiro amewatahadharisha vijana hao kutokubeba ajenda ambazo hawazielewi kwa undani wake kwa kuwaeleza wasifanye jambo ambalo halina faida kwao wala kwa Taifa.

"Serikali ya Awamu ya Tano na Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa na Rais Magufuli ana imani kubwa na  vijana,unapokuwa kijana wa CCM unapaswa kuwa mzalendo,uwe na adabu na heshim.Kataa rushwa na kubwa zaidi tufanye kazi kwa bidii.

"Linapotokea jambo tusishabikie pasipo kuelewa undani wa jambo hilo kwani hakuna kitu kibaya kama watu wasioitakia mema nchi yetu kutaka kukuingizia wewe kijana katika ajenda zao ambazo wewe huzifahamu kwa ajili ya kuharibu amani,"amesema.

Makwiro amewakumbusha vijana kutambua wao ndo nguvu na jeuri ya CCM katika kufanikisha mambo yote yanayopaswa kufanyika katika chama hicho na kueleza kujiandaa na uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika mwaka ujao.

"Tuhakikishe tunajiandaa kwenye uchaguzi huo mapema na vijana mnayo nafasi ya kuwania nafasi za uongozi kwenye Serikali za mitaa.Hivyo ni jukumu letu vijana wa CCM kuanza kujipanga mapema ili tushinde kwa kishindo,"ameongeza.

Pia amekumbusha umuhimu wa vijana kuchangamkia fursa ya mikopo na kwamba Serikali kutoa fedha mikopo kwa vijana wote ili kufanya shughuli za kimaendeleo na kuwashauri vijana kutengeneza vikundi ili kufanya ujasiriamali.

"Itapendeza pia kama mtakuwa na CV(wasifu) zenye maelezo yao ya taaluma na vipaji mlivyonavyo na kuziwasilisha katika ofisi ya wilya ya umoja huo wa vijana ili hata nafasi za kazi zikitokea wilayani na kwingineko itakuwa rahisi kupata ajira serikalini na maeneo mengine,"amesema.

Makwiro amewaahidi vijana wilayani Kibiti kuwa kwa kumchagua yeye kuwa Mwenyekiti UVCCM Mkoa wa Pwani pamoja na wajumbe wa baraza kuu la mkoa huo atahakikisha anatumia rasirimali zake binafsi, akili zake kuhakikisha jumuiya hiyo ya vijana inatatua baadhi ya changamoto za vijana hao,"amesema.

Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa Mkoa wa Pwani,Ramadhan Mlao amesema yupo bega kwa bega na Makwiro ili kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Mwenyekiti wa umoja huo taifa, Kheri James kuwasaidia vijana kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza kwa niaba ya wajumbe wa baraza la wilaya hiyo, Mwenyekiti UVCCM wa Kibiti,Juma Ndaluke amesema wamepokea maelekezo yote kutoka kwa viongozi hao wa Mkoa na ameahidi kuyatekeleza kwa jinsi watakavyojaliwa huku akisisitiza yeye na  wajumbe wake hawatowaangusha katika uboreshaji wa utendaji kazi wa umoja huo wa vijana.
  Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani, Charangwa Seleman Makwiro (katikati) akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa baraza la umoja wa vijana (UVCCM) Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani. Kushoto ni Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa wa Mkoa wa Pwani,Ramadhan Mlao na Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Kibiti,Juma Ndaluke. Picha zote na Elisa Shunda
   Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani, Charangwa Seleman Makwiro (katikati) akimkabidhi Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Kibiti, Juma Ndaluke (wa pili kulia) kadi 200 na kanuni 100 kwa baada ya kuzungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa baraza la umoja wa vijana (UVCCM) Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani. Wa kwanza kushoto ni Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa wa Mkoa wa Pwani ,Ramadhan Mlao.
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Kibiti, Juma Ndaluke akizungumza katika mkutano huo. 
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani, Charangwa Seleman Makwiro (katikati) akimkabidhi Yusuph Kimbe (kulia) kadi ya Umoja wa Vijana baada ya kujiunga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...