THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

NEWS ALERT:WAWILI WAPOTEZA MAISHA,MKURUGENZI TBC ANUSURIKA KIFO KUFUATIA AJALI YA GARI WILAYANI KASULU,MKOANI KIGOMA


Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

Watu wawili wamefariki Dunia wilayani Kasulu mkoani Kigoma kufuatia ajali ya gari la Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC Dkt. Ayub Rioba, lililokuwa likitokea wilayani Kibondo kwenda Kigoma Mjini.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kigoma, Kamishna Msaidizi Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni utelezi uliosababisha gari kuacha njia na kuwagonga waenda kwa miguu watatu.

Kamanda  Otieno aliwataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni watembea kwa miguu wawili, waliofahamika kwa majina ya Teresia Mpoma (55) mkulima na Mkazi wa Nyakitonto, Yuster Masharubu (55) mkazi wa Nyakitonto na Majeruhi mmoja aliefahamika kwa jina la Diana Shedrack (10) mwanafunzi shule ya Msingi Nyakitonto, ambae hali yake ilielezwa kuwa mbaya huku akiendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Kasulu.

Amesmea Gari la Mkurugenzi Mkuu wa TBC lililopata ajali lenye namba za usajili STK 8769 lilikuwa na abiria wawili akiwemo mkurugenzi mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba na Mkuu wa kanda ya magharibi TBC Mhandisi Zebron Mafuru ambao wote wametoka salama na hali zao ni nzuri.

Kamanda Otieno aliongeza kuwa kutoa tahadhari kufuatia  Chanzo cha ajali hiyo kuwa ni utelezi unaotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha Katika Mkoa huo,hivyo amewaomba madereva kuendesha magari kwa umakini kutokana na ubovu wa barabara hiyo na kuzingatia sheria za barabarani.

Dkt. Rioba yuko katika ziara ya kukagua vituo vipya vya matangazo vilivyojengwa katika maeneo ya mipakani.

 Pichani kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba baada ya kunusurika kifo akiwa eneo la tukio pamoja na Polisi waliofika ku
 Gari la Mkurugenzi Mkuu wa TBC lililopata ajali lenye namba za usajili STK 8769 lilikuwa na abiria wawili akiwemo mkurugenzi mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba na Mkuu wa kanda ya magharibi TBC Mhandisi Zebron Mafuru ambao wote wametoka salama na hali zao ni nzuri.

.