THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

NGORONGORO HEROES YAINGIA KAMBINI

Kikosi cha timu ya Taifa chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) kimeingia kambini kujiandaa na mchezo wake wa raundi ya kwanza ya kuitafuta tiketi ya kucheza fainali za vijana za Africa dhidi ya Congo mchezo utakaochezwa Machi 31, 2018 kwenye Uwanja wa Taifa.
Timu ya Taifa ya Tanzania chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) wanatarajia kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa na Morocco ,mchezo utakaochezwa Machi 17, 2018 kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. 
Mchezo huo ni wa kujiandaa na mchezo wa kuitafuta tiketi ya kucheza fainali za Africa kwa Vijana dhidi ya DR Congo utakaochezswa Machi 31, 2018. 
Morocco wanatarajia kutua Tanzania Machi 14,2018 ikiwa na msafara wa watu 31 wanaojumuisha wachezaji 23 na viongozi 8 wa benchi la ufundi. 

Mchezo huo utachezwa saa 10 jioni.
Kikosi kilichoingia kambini makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Machi 6, 2018 ni wachezaji 40 ambao watapunguzwa na kubaki wachezaji 30 baada ya kumalizika wiki ya kwanza ya mazoezi.

Kikosi kilichoingia kambini: 
1.Ramadhan Kabwili(Young Africans), 2.Abutwarib Mshedi(Mtibwa), 3.Johny Kwiyenda(Makongo), 4.Ally Salim (Simba)
5.Kibwana Ally Shomari(Mtibwa), 6.Ally Hussein Msengi(Mbao)
7.Enrick Vitalis Nkosi(African Lyon), 8.Dikson Job(Mtibwa)
9.Assad Juma(Singida United), 10.Said Mussa Bakary(Young Africans)
11.Ally Ng’anzi(Singida United), 12.Kelvin Nashin Naftal(JKT Tanzania)
13.Shaban Ada(Lipuli), 14.Issa makamba(Singida United)
15.Mohamed Rashid(Singida United), 16.Marko Gerald(JMK)
17.Syprian Mtesigwa(Dodoma FC), 18.Muhsin Makame(Njombe Mji)
19.Yohana Mkomola(Young Africans), 20.Ibrahim Abdallah (Miembeni City) na 21.Abdul Suleiman(Ndanda).
Wengine ni: 22.Nickson Kibabage(Njombe Mji) ,23.Mussa Najimu(Changanyikeni),24.Maziku Aman(Makongo), 25.Hamis Mustafa(Ndanda), 26.Samson Myati(Toto Africans)
27.Said Mohamed(Azam FC), 28.Ayoub Mohamed(Young Africans)
29.Mohamed Mussa(Azam FC), 30.Emanuel Myati(Tz Prisons)
31.Riffat Hamis(Mtibwa), 32.Oscar Masai(Azam FC)
33.Paul Peter(Azam FC), 34.Vitalis Mayanga(African Lyon) na35.Rajab Mohamed(Azam FC).
Wengine ni: 36.Pontia Ohonya, 37.Maka Anthony(Young Africans)
38.Israel Mwenda(Alliance), 39.Hance Msonga(Alliance) na 40. Moses Kitandu(Simba)