SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imetenga shilingi bilioni 5 kwa ajili ya kununua mashine za kupima vipimo vya ugonjwa wa kifua kikuu katika zahanati na vituo vya afya nchini. 

Hayo yamezungumzwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa dawa za kutibu ugonjwa wa Kifua Kikuu kwa watoto kuanzia umri wa miaka 14 kushuka chini leo jijini Dar es salaam. Serikali imadhamiria kupambana na ugonjwa wa Kifua Kikuu hivyo tumetenga shilingi bilioni 5 kwa ajili ya kuongeza mashine nyingine za kufanya uchunguzi kwa haraka vya ugonjwa wa Kifua Kikuu zinazoitwa Genexpert " alisema Waziri Ummy. 

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa marufuku kwa watoa huduma kutoa matibabu ya Kifua Kikuu kwa gharama yoyote kwani huduma hiyo ni bure. Kwa mujibu wa Waziri Ummy amesema kuwa marufuku kwa waganga wa kienyeji kuwashikilia wagonjwa wa Kifua kikuu na badala yake wawaruhusu waende hospitali kwa ajili ya msaada wa haraka. 

Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa takriban watu laki moja na 60 wana maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu kwa makadirio ya mwaka 2016. Sambamba na uzinduzi wa dawa hizo Waziri Ummy amegawa mashine nyingne za Genexpert kwa ajili ya kufanyia uchunguzi wa makohozi ili kugundua kuna maambukizi au hapana kwa hospitali za ,Kairuki, Agakhan, Regency , TMJ na Indumandal ambazo kila mashine moja inagharimu shilingi milioni 34 .

Aidha Waziri Ummy ametoa rai kwa wazazi na walezi wa watoto kwenda hospitali mara wanapoona dalili moja wapo ya TB ikiwemo kuumwa mara kwa mara kwa muda wa wiki mbili, kukosa furaha, mtoto kulia mara kwa mara, kupungua uzito , kuchelewa kukua na kikohozi cha mara kwa mara. 
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto akionyesha dawa kutibu Kifua Kikuu kwa watoto wadogo wakati wa uzinduzi wa dawa hiyo leo jijini Dar es salaam kueleka maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu tarehe 24 Machi 2019.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na baadhi ya wadau wa Sekta ya afya hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa dawa ya kutibu kifua kikuu kwa watoto wadogo kueleka maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu tarehe 24 Machi 2019.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kushoto akimuangalia mtoto Salome katikati akinywa dawa ya Kifua Kikuu wakati wa uzinduzi wa dawa ya kutibu kifua Kikuu kwa watoto wadogo leo jijini Dar es salaam, kutoka kulia ni Mratibu wa Kupambana na Magonjwa ya Kifua Kikuu na Ukoma Dkt. Beatrice Mutayoba, anayefuata aliyevaa kitenge ni mzazi wa Salome Bi. Upendo Jeremiah.
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Mohammed Bakari Kambi baadhi ya wadau wa Sekta ya afya hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa dawa ya kutibu kifua kikuu kwa watoto wadogo kueleka maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu tarehe 24 Machi 2019 iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wadau wa Sekta ya afya wakifuatilia kwa makini Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu hayupo pichani wakati wa uzinduzi wa dawa ya kutibu kifua kikuu kwa watoto wadogo kueleka maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu tarehe 24 Machi 2019 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...