Na Genofeva Matemu - WHUSM
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe ameahidi kufikisha taarifa ya hatua ambayo Tanzania imefikia katika harakati za kutafiti na kuhifadhi kumbukumbu za ukombozi wa Bara la Afrika kwa mawaziri wa utamaduni wa nchi za kusini mwa Afrika ili nchi hizo wanachama ziweze kuendelea na hatua nyingine ya kuchangia katika ujenzi wa kituo cha kuhifadhi kumbukumbu hizo.
Waziri Mwakyembe ameyasema hayo leo Mkoani Mbeya alipofanya ziara kukagua maeneo yaliyotumika wakati wa harakati za ukombozi wa Bara la Afrika na kusema kuwa serikali ipo katika mpango ambao maeneo yaliyotumika katika harakati za ukombozi wa Bara la Afrika yatakarabati na kurejesha muonekano wake wa awali ili yasipotezi historia.
“Majengo yaliyotumika katika harakati za urithi wa ukombozi wa Bara la Afrika ni sehemu ya historia na maeneo muhimu sana ambayo yanatakiwa kuboreshwa ili yaweze kuendelea kuwepo katika muonekano ule ule wa awali kwa lengo la kutokupoteza historia yake” amesema Mhe. Mwakyembe
Aidha Mhe. Mwakyembe amesema kuwa serikali imechukua wajibu wake wa kubaini maeneo yaliyotumika wakati wa harakati za ukombozi wa Bara la Afrika na kuwaomba viongozi wote nchi nzima kuendelea kubaini maeneo na vitu vilivyotumika katika harakati za ukombozi wa Bara la Afrika vilivyopo katika maeneo yao ili wizara   iyaendeleze kwa maslahi ya taifa na Afrika kwa ujumla.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Paul Ntinika (kulia) wakati wa ziara yake leo Mkoani Mbeya kutembelea maeneo ya urithi wa ukombozi wa Bara la Afrika
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto mwenye miwani) akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Paul Ntinika (kulia mwenye miwani ) alipotembelea eneo la Game lililotumika kama kambi ya wapigania uhuru wa Msumbiji leo Mkoani Mbeya wakati wa ziara yake kutembelea maeneo ya urithi wa ukombozi wa Bara la Afrika
Nyumba zilizopo katika eneo la Game zilizotumiwa na wapigania uhuru wa Msumbiji ambazo kwa sasa zinatumiwa na Idara ya Maliasili na utalii.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akimsikiliza Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika Bibi. Ingiahedi Mduma (kulia) alipotembelea Nyumba ya Binti Matola aliyekuwa mwanaharakati na rafiki wa Mwalimu Nyerere ambaye aliweza kumhifadhi Hayati Mwalimu Nyerere wakati wa kupigania uhuru wakati wa ziara yake kutembelea maeneo ya urithi wa ukombozi wa Bara la Afrika leo Mkoani Mbeya.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...