Mshauri mteule wa masuala ya usalama Marekani, Bolton John (69).

Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii
RAIS  wa Marekani, Donald Trump amemteua  Bolton John (69) kuwa Mshauri wa masuala ya usalama baada ya kumwachisha kazi aliyekuwa katika nafasi hiyo H.R  McMaster.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Rais Trump ameandika kumteua Bolton John (69) kuwa mshauri wake wa masuala ya usalama wa taifa na mteule huyo kuanza kazi rasmi ifikapo mwezi Aprili.

Inasemekana kupishana kauli kati ya Trump na McMaster siku za nyuma  ndiko juu ya sera za nchi hiyo ndiko kulikopelekea maamuzi ya Rais Trump kumfukuzisha kazi.

John Bolton anakuwa mshauri wa tatu wa masuala ya usalama huku akiwa amehudumu katika mihula kadhaa na aliwahi kuhudumu kama mwakilishi wa Marekani Umoja wa Mataifa.

McMaster ataungana na aliyekuwa Waziri wa mambo ya Nje, Rex ambaye alifutwa kazi siku chache zilizopita kutokana na maamuzi ya Rais Trump.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...