Walimu wanaopatiwa mafunzo ya siku nne ya ujasiriamali yanayotolewa na Shirika la Sayansi, Elimu na Utamaduni la Umoja wa Mataifa(UNESCO) chini ya ufadhili wa program ya Malala wametakiwa kuhakikisha wanatumia elimu waliyopata kuwafanya wanafunzi hasa wa kike kujitambua na kukamilisha malengo yao.

 Kauli hiyo imetolewa na Ofisa Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu wakati akifungua semina hiyo inayoshirikisha wajumbe 64 wakiwemo walimu 40 na wakuu wa Shule 20 na maofisa elimu wanne kutoka wilaya nne za mkoa wa Tanga. Wilaya zinazohusika ni za Pangani, Muheza, Korogwe na Lushoto. Semina hiyo ni sehemu ya mradi wa kuwafanya watoto hasa wa kike kujitambua, kupunguza utoro na mimba za utotoni ili kufikia malengo yao ulioanza mwaka 2015.

 Mayasa alisema kwamba ili wawasaidie watoto hao wamalize masomo yao ni vyema walimu hao wakatambua umuhimu wa mafunzo hayo na kuwa karibu na watoto na kuishi nao kutambua shida zao na kuwasaidia kukabiliana nazo ili waweze kusonga mbele. Alisema kama walimu wakiamua kufanyakazi ya kufundisha tu bila kuwa karibu na watoto dhima ya kuwasaidia kufikia malengo hata ya kujiajiri wenyewe wakimaliza masomo haitafikiwa.

 Aliwataka walimu hao kusogeza elimu yao kwa wenzao na katika hilo kuweza kusaidia kufanya vyema kwa watoto katika masomo na pia utayari wa maisha. Aliwakumbusha walimu kusikiliza watoto kutambua shida zao na kujua namna ya kuwasaidia badala ya kubaki kulalamika kwamba watoto hao ni wakorofi au wanakiuka kanuni za shule. Alisema alishawahi kutembelea shule moja na kukuta mtoto ambaye anachelewa kufika shule lakini alipohoji aligundua kwamba kijana huyo wa kidato cha nne ana mama mgonjwa mahututi na lazima amhudumie kwa kuwa baba yake alikwishafariki.

Ofisa Mradi wa Shirika la Sayansi, Elimu na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Jennifer Kotta akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa mafunzo ya siku nne ya ujasiriamali yanayotolewa na UNESCO chini ya ufadhili wa program ya Malala yanayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hospitali ya rufaa ya Bombo, mkoani Tanga.

Mgeni rasmi Ofisa Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu akitoa nasaha wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku nne ya ujasiriamali yanayotolewa na UNESCO chini ya ufadhili wa program ya Malala yanayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hospitali ya rufaa ya Bombo, mkoani Tanga. Kushoto ni Ofisa Mradi wa Shirika la Sayansi, Elimu na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Jennifer Kotta na kulia ni Simon Mombeyi kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi, wa Idara ya Elimu.

Sehemu ya washiriki wa mafunzo ya siku nne ya ujasiriamali yanayotolewa na UNESCO chini ya ufadhili wa program ya Malala wakisikiliza kwa umakini nasaha za mgeni rasmi (hayupo pichani) yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Hospitali ya rufaa ya Bombo, mkoani Tanga.

Simon Mombeyi kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi, wa Idara ya Elimu akizungumza jambo na washiriki wa mafunzo ya siku nne ya ujasiriamali yanayotolewa na UNESCO chini ya ufadhili wa program ya Malala yanayofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hospitali ya rufaa ya Bombo, mkoani Tanga.

Mkufunzi wa mafunzo ya ujasiriamali kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO), Jacqueline Stenga akiendesha mafunzo ya siku nne ya ujasiriamali yanayotolewa na UNESCO chini ya ufadhili wa program ya Malala kwa wajumbe 64 wakiwemo walimu 40 na wakuu wa Shule 20 na maofisa elimu wanne kutoka wilaya nne za mkoa wa Tanga yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Hospitali ya rufaa ya Bombo, mkoani humo.

Mgeni rasmi Ofisa Elimu wa mkoa wa Tanga, Mayasa Hashimu (wan ne kushoto) katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya siku nne ya ujasiriamali yanayotolewa na UNESCO chini ya ufadhili wa program ya Malala kwa wajumbe 64 wakiwemo walimu 40 na wakuu wa Shule 20 na maofisa elimu wanne kutoka wilaya nne za mkoa wa Tanga yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Hospitali ya rufaa ya Bombo, mkoani humo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...