Na  Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
CSHIRIKA la Reli Nchini (TRC) imeingia mkataba wa ununuzi vichwa vya trein 11 na kampuni ya Progress Rail Locomotives (PRL) ya Marekani ili kuweza kuongeza idadi ya vichwa katika shirika hilo
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo,  Masanja Kadogosa amesema kuwa ununuzi wa vichwa hivyo itafanya shirika kuwa vichwa 47.
Amesema walikuwa na vichwa 29 ambavyo kwa mahitaji vilikuwa havitoshi lakini kwa sasa shirika linatakuwa vichwa vya kutosha katika kutoa huduma nzuri kwa wateja wa Trein.
Amesema kuwa vichwa vitafanya majaribio katika awamu tatu ambapo ya kwanza ni kuangaliwa na watalaam katika ubora wake na awamu nyingine kuviwasha na kupakia tani 700 toka Dar es Salaam pamoja na hatua ya tatu kupakia tani 1200 toka  Morogoro hadi Kigoma na Mwanza.
Kadogosa amesema serikali imeokoa zaidi dola 8,800,000 kwa  kila kichwa kutoka dola 3 200,000 kutokana na na mazungumzo ya kamati.
 Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa Meneja wa Kanda wa Nchi za Afrika zilizo Jangwa la Sahara wa Kampuni ya Progress Rail Caterpillar, Barend Hanekom wakibadilishana mikataba mara baada ya kutiliana saini ya makubaliano 
Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa Meneja wa Kanda wa Nchi za Afrika zilizo Jangwa la Sahara wa Kampuni ya Progress Rail Caterpillar, Barend Hanekom wakionesha mikataba kwa waandishi habari mara baada ya kusaini jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...