Na Agness Francis, Globu ya jamii
UONGOZI wa Singida United umekana kufungiwa kwa mchezaji wa timu yao Danny Lyanga kwa kosa la kusaini mikataba timu mbili.
Taarifa
zilizoenekana kupitia kwa vyombo mbalimbali vya habari, ikielezea kuwa
Lyanga amefungiwa na Shirikisho la Mpira duniani (FIFA) kutokana na
kudaiwa kusaini kuzitumikia timu mbili ambazo ni Singida United na Fanja
Fc ya Oman.
Hivyo FIFA na kuamua kumfungia mchezaji huyo Danny Lyanga kwa muda wa miezi sita kwa kosa la kusaini mkataba timu mbili.
Ambapo inasemekana kuwa alisaini mkataba na Singida United wakati wa
dirisha dogo akiwa bado ana mkataba wa miaka miwili na klabu ya Fanja FC
ya Oman.
Hata hivyo uongozi wa Singinda United umekananusha uvumi huo na kusema si kweli.Umefafanua
Lyanga ni mchezaji wao halali wamemsajili kutoka Fanja Fc ya Oman na
kufanya makubaliano ya mkataba ambao ulionyesha kuwa mchezaji huo
ameshamalizana na kikosi hicho na kuwa huru kununuliwa na Timu
nyingine.
Imeelezwamchezaji hiyo hajafungiwa na FIFA miezi 6
kama inavyodaiwa. Kilichotokea mpaka kupelekea uvumi huo kusambaa katika
vyombo mbalimbali vya habari ni kuchelewa kupata kibali cha kuchezea
nje ya Nchi (ITC) kutoka Fanya Fc.
"Kilichotokea ni kwamba
ITC ya Danny Lyanga iljchelewa kuja kutokana na dirisha la usajili
kufungwa, hivyo FIFA walituandikia barua sisi pamoja na TFF kwamba ITC
ya Lyanga itakamiIika hadi hapo dirisha kubwa la usajiri
litakapofunguliwa hapa Tanzania kuanzia Julai 2018.
"Hivyo basi
Danny Lyanga hajafungiwa na hivi tunategemea kumtumia kwenye Michuano
ambayo klabu yetu itakwenda kushiriki nje ya Nchi"amesema msemaji wa
uongozi huo.Uongozi umesema "Tunaomba vyombo vya habari kutumia taarifa
rasmi kutoka vyanzo rasmi kwa ajili ya maslai ya Mpira wa miguu hapa
nchini".
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...