THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

KESI YA MHASIBU WA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI MSUMBIJI YAPIGWA KALLENDA.

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii
UPANDE wa mashtaka katika kesi ya utakatishaji fedha wa dola za Marekani 150,000 inayomkabili Mhasibu wa Ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji Joyce Moshi, umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa wameiandikia barua nchi hiyo kuiomba msaada wa kisheria.

Wakili wa Serikali, Wankyo Simon ameeleza hayo leo,mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa.

Wakili Wankyo amedai, upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika, ila wameandika barua kwenda nchini Msumbiji kuomba msaada wa kisheria (Mutual Legal Assistance) ili kufanya upelelezi wa kesi hiyo.

Kutokana na maelezo hayo, Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi Machi 27 mwaka 2018.

Mshtakiwa Mushi anakabiliwa na mashtaka 9, ikiwemo kughushi na utakatishaji fedha.

Inadaiwa Okbota 25,mwaka 2016 katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania zilizopo Maputo nchini Msumbiji, alighushi barua ikionesha kuwa Ubalozi wa Tanzania nchini humo umeielekeza Benki ya Millennium kupeleka dola za Marekani 10,000 katika akaunti inayomilikiwa na Joyce Moshi akijua yakuwa si kweli.

Pia anadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Oktoba 25, mwaka 2016 na Aprili 12 mwaka 2017 mshtakiwa akiwa mtumishi wa umma kama Mhasibu wa Ubalozi wa Tanzania aliiba dola za Marekani 150,000 mali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia inadaiwa kati ya Okbota 25, mwaka 2016 na Aprili 12, mwaka 2017 katika ofisi za ubalozi huo, Moshi alijipatia dola za Marekani 150,000.


Pia inadaiwa kati ya Oktoba 25, mwaka 2016 na Aprili 12, mwaka 2017 katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania uliopo Maputo nchini Msumbiji na Benki ya Millenium BIM tawi la Julius Nyerere Maputo, alijipatia dola za Marekani 150,000 wakati akijua fedha hizo ni zao la kughushi.