Unaweza kuwa wewe, ndugu yako,rafiki au jamaa yako ameunganishwa katika kesi ya
mauaji. Aghalabu, daktari anasubiriwa kutoa ushahidi mahakamani kuhusu sababu
za kifo cha marehemu.
Na ni ushahidi huo wa daktari utakaokuondoa katika
kesi hiyo ya mauaji au utakuingiza
katika kesi hiyo na hivyo kutiwa hatiani na kuadhibiwa.
Lakini sio daktari tu bali wenye kesi wote ambao ushahidi
wake unahitaji mtaalam(expert) kuthibitisha mfano mkemia, mtaalam wa muandiko
na sahihi, mtaalam wa biashara , mtaalam wa DNA
nk.
1.USHAHIDI WA DAKTARI.
Kifungu chac 47 cha Sheria ya Ushahidi kinaruhusu kutumika na
kukubalika kwa ushahidi wa mtaalam( expert). Mtaalam ni pamoja na daktari.
2. MAMBO 6 MUHIMU UNAYOTAKIWA KUJUA.
A ).
Kabla daktari au mtaalam mwingine yoyote hajaanza kutoa ushahidi wake ni
ni muhimu sana athibitishe kwa ushahidi kuwa yeye ni mtaalam kweli (expert) kwa
hicho anachotaka kutolea ushahidi. Usikubali akaanza kueleza kabla ya kuthibitisha utaalam.Mtake
athibitishe hilo kwanza.
Utaalam unathibitishwa kwa taaluma(professional). Kama ni
daktari na mtaalam wa eneo fulani la tiba ,mfano mifupa, moyo, nk, aoneshe
cheti cha taaluma katika eneo hilo. Halikadhalika kwa wataalam wengine nao
wanatakiwa kufanya hivyo. Kama hawezi kuthibitisha hilo basi hiyo ni faida
kwako kwakuwa ushahidi wake ni wa kutia shaka.
Na hapo haijalishi mtaalamu(expert) huyo ameletwa na nani.
Awe ameletwa na polisi, PCCB, au idara nyingine yoyote. Msimamo huu ulitolewa
na mahakama katika kesi ya MUHAMMED
AHMED V
REPUBLIC(1957)E.A. C.A 523.
B ). Daktari au shahidi yoyote mtaalam,
asiwe tu mtaalam wa vyeti, bali awe mwenye ujuzi wa uzoefu wa kazi husika. Kwa
mfano, daktari au mtaalam ambaye amemaliza chuo, ana cheti lakini hajaajiriwa
wala kuwahi kuifanyia kazi taaluma yake popote hawezi kuitwa mtaalam mwenye
uwezo(competence) wa kutoa ushahidi wa kitaalam.
KUSOMA ZAIDI
sheriayakub.blogspot.com
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...