Rais wa Urusi Vladimir Putin wa Chama cha Independent.

Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii
RAIS wa Urusi Vladimir Putin wa Chama cha Independent kwa mara nyingine ameibuka mshindi wa kiti cha urais kwa muhula mwingine wa miaka sita.

Putin ameibuka na ushindi mnono wa zaidi ya asilimia 77, akiwamwaga Pavel Grudinin wa Communist party na Vladmir Zhirinovsky wa Chama cha "LDPR" katika uchaguzi uliofanyika jana Machi 18 mwaka huu.

Putin (65) alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuongoza taifa hilo mwaka 2000 ambapo alihudumu kwa mihula miwili na akachaguliwa kuwa Waziri Mkuu kwa muhula mmoja.

Mwaka 2012 Putin   alichaguliwa kuwa Rais na ni kipindi ambacho mihula ya uongozi iliongezwa kutoka miaka 4 hadi 6.

Ushindi huo unamfanya Vladimir Putin kwa Rais wa urusi hadi 2024.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...