Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
KADIRI kengele inavyogonga kuashiria sikukuu ya Pasaka ipo jirani, ndivyo dhahiri kuwa siku za kuelekea Tamasha la Pasaka zinahesabika. Ni Aprili Mosi, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.
Tumezoea mara nyingi kushuhudia Tamasha la Pasaka likifanyika jijini Dar es Salaam lakini waandaaji wa tamasha hilo wameamua mwaka huu iwe zamu ya Kanda ya Ziwa. Hivyo Pasaka hii, watu wa Kanda ya Ziwa watahemewa kwa burudani ya nyimbo zenye kumsifu na kumtukuza Mungu na litanenwa neno la Mungu.
Hivyo Aprili Mosi ni CCM Kirumba, Aprili Pili Tamasha la Pasaka litachukua nafasi kwenye Uwanja wa Halmashauri, mkoani Simiyu. Hakuna ubishi tena katika sikukuu ya Pasaka mwaka huu wakazi wa Kanda ya Ziwa, eneo ambalo litakuwa sahihi kwao kuisheherekea siku hiyo ni kwenye Tamasha la Pasaka.
Wakati siku zikikaribia kuelekea Tamasha la Pasaka kwa mkazi wa Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa jumla ni kuendelea kumuomba Mungu ili aendelee kukupa uzima na afya njema.Waandaaji wa tamasha hilo, Kampuni ya Msama Promotion, mwaka huu wameamua kuweka vionjo tofauti ili kuhakikisha tamasha hilo linafanyika na  kuacha historia kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa.
 Kila mwanamuziki aliye kwenye chati, nyimbo zake za kumsifu na kumtukuza Mungu zikiwa zinatamba na kusikika, atakuwemo kuburudisha mashabiki wake.Kwa mujibu wa waandaji wa Tamasha la Pasaka, kati ya wengi watakaofanya kweli, atakuwepo mwanamuziki maarufu nchini Rose Mhando na wengine zaidi ya 15 kutoka ndani na nje ya nchi.Inafahamika kuwa Rose Muhando huwa hahitaji utambulisho. Ni mwanamuziki mwanamuziki mkubwa ambaye Muumba wa Mbingu na Ardhi amemjaalia kipaji cha kuimba kilichoambatana na sauti maridadi. Muziki wa Rose Mhando unapopigwa wapo ambao wanasimamisha shughuli zao kwa muda.
Natamani kutaja baadhi ya nyimbo zake atakazoimba siku hiyo lakini acha nikae kimya. Sitaki kukumalizia uhondo. Vema ufike CCM Kirumba kisha Uwanja wa Halmashauri, Simiyu ili macho na masikio yako yapate kumuona na kumsikiliza Rose Mhando. Uwezo wake wa kuimba umemfanya awe nyota ya muziki wa Injili.Kwa Rose Mhando mwenyewe anajua ukubwa wa Tamasha la Pasaka. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...