Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

JUMLA ya wanachama 27 wa Chadema wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi(CCM)wilayani Kakonko mkoani Kigoma kutokana na kuvutiwa na utendaji kazi wa Serikali ya CCM.

Wanachama hao wamejiunga leo katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Wilaya kilichoendeshwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole.

Wakizungumza baada ya kukabidhiwa kadi na kiongozi huyo,wanachama hao wapya wamesema wamefikia uamuzi huo baada ya kuguswa na kazi zuri inayofanywa na CCM na kukosa demokrasia Katika chama chao cha Chadema kwa madai kipo kwa ajili ya watu wachache.
Riberatusi Kamamba ni mmoja kati ya wanachama wa Chadema waliohamia CCM ambapo ameeleza ameamua kuhamia katika chama hicho kutokana na utendaji kazi na utekelezwaji wa ilani ya chama hicho unavyo fanya na Rais wa Chama hicho anavyo hakikisha fedha za Serikali zinatumika ipasavyo.

Amesema mwanzoni viongozi walikuwa hawana utaratibu wa kuwatembelea wananchi na kuangalia changamoto wanazo kutana nazo na kukagua miradi ya maendeleo."Lakini kwa sasa Chama hicho kinafanya kazi hiyo na kuhakikisha kinawachukulia hatua wale wote wanaotumia fedha za Serikali kwa matakwa yao binafsi na watumishi wote wanatembelea wananchi kutatua kero," amesema.

Nae Gidioni Ruhaga aliekuwa Muasisi wa Chadema amesema ana mambo mengi yaliyomfanya ahamie katika chama hicho,miongoni mwa mambo hayo ni sera zilizopo CCM.Amesema kwa sasa chama hicho kimerudisha heshima na utaratibu uliokuwa nao ni na kinajali demokrasia na hakina ubaguzi.Amesema chama alichokuwa akikitumikia kimekuwa kinaubaguzi na hakiwajali wanachama wanaopigana kukiweka madarakani na ni wakwanza kuipinga Serikali haitendi haki lakini hata wao hawafanyi hivyo.
"Na wamekuwa wa kwanza kujinufaisha na fedha zinazotolewa kwaajili ya kukiendesha chama hicho," amesema.Akizungumza na wanachama waliojitokeza katika kikao hicho Polepole amesema amesikitishwa na kitendo kilicho fanywa na upinzani cha kuwafungia ndani madiwani wote wa chama hicho na kuwanyang'anya simu zao kwa kuhofia watahamia Chama tawala .

Amesema viongozi hao baada ya kusikia yakuwa kuna ugeni wa kiongozi huyo waliamua kuwaweka ndani madiwani na kueleza kila mwananchi anahaki ya kuhamia chama chochote anacho kitaka hata wao wamewaachia viongozi na wanachama wengine kuhamia chama wanacho kihitaji."Imeandikwa hata kwenye vitabu vya dini alaaniwe anae muogopa mwanadamu nimeshangaa sana watu wanatuogopa hadi wanaamua kuwaficha madiwani wao.
"Ssi hatutamnunua mtu kwa gharama yeyote ile hata huyo Mbunge wenu akija kwetu hatumuhitaji, tunahitaji wananchi wanaoamua wenyewe kujiunga na Chama tawala kwa kuona utendaji kazi na misingi ya chama chetu", amesema Polepole.730236

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...