Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

WANANCHI wengi wamesema wana imani kubwa na taarifa zinazotolewa na Rais kwa asilimia 70  na Waziri Mkuu kwa asilimia 64 huku idadi ndogo zaidi wanamwamini mwenyekiti wao wa kijiji kwa asilimia 30, wabunge  wa chama tawala asilimia 26 na  wa upinzani asilimia 12 wakati viongozi wa Serikali kwa ujumla ya asilimia 22.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze wakati anatoa matokeo ya Twaweza yalitokana na utafiti uliofanyika uliojukana kama muhtasari  uitwao Siyo kwa kiasi hicho? 

Pia maoni ya wananchi kuhusu taarifa na mijadala ambapo Eyakuze anafafanua takwimu za muhtasari huo zinatokana na utafiti wa Sauti za Wananchi ambao huratibiwa na taasisi ya yao.Sauti za Wananchi ni utafiti wenye uwakilishi wa kitaifa unaotumia simu za mikononi.

"Matokeo ya utafiti unaonesha wananchi wengi kuwa na imani kubwa na taarifa zinazotolewa na Rais na Waziri Mkuu,"amesisitiza.

Pia amesema wananchi wanaendelea kuunga mkono kwa kiwango kikubwa upatikanaji wa taarifa ambapo  wananchi 7 kati ya 10 wanasema taarifa zinazomilikiwa na mamlaka za umma ni mali ya umma ni asilimia 70 juu zaidi kutoka asilimia 60 mwaka 2015).

"Na wananchi 9 kati ya 10 wanasema wananchi wa kawaida wapate taarifa zinazomilikiwa na mamlaka za umma kwa asilimia 86  juu zaidi kutoka asilimia 77  mwaka 2015) na kwa kuwapa wananchi uwezo wa kupata taarifa kunaweza kupunguza rushwa asilimia 86 , juu zaidi kutoka asilimia 80 mwaka 2015.

"Pamoja na kuunga mkono kwa kiwango kikubwa upatikanaji wa taarifa, wananchi 9 kati ya 10 hawajawahi kuomba taarifa kutoka katika ofisi za serikali kwa asilimia 95 , mamlaka za maji asilimia 93 , au vituo vya afya  asilimia 93,"amesema. 

Ameongza utafiti unaonesha kuwa wananchi wameendelea kutumia vyanzo vile vile vya habari bila kuwa na mabadiliko makubwa isipokuwa kwa upande wa runinga ambapo mwaka 2013 runinga ilikuwa ni chanzo kikuu cha taarifa kwa asilimia 7 ya wananchi na mwaka 2017 ni asilimia 23 ya wananchi. 

Eyakuze amesema hata hivyo imani kwa aina mbalimbali za vyanzo vya habari inashuka .Radio kutoka asilimia 80 mwaka 2016 hadi asilimia 64 mwaka 2017, runinga kutoka asilimia 73 mwaka 2016 hadi asilimia 69 mwaka 2017 na maneno ya kuambiwa kutoka asilimia 27 mwaka 2016 hadi asilimia 13 mwaka 2017.

 "Pamoja na kushuka kwa imani na vyombo vya habari, wananchi bado wanaunga mkono uhuru wa vyombo vya habari kwani  wananchi wanasema gazeti lililochapisha taarifa za uongo ama zisizo sahihi liombe radhi na kuchapisha marekebisho ni asilimia 62 badala ya gazeti hilo kufungiwa ama kutozwa faini asilimia 38. 

"Idadi kubwa ya wananchi pia wanasema kuwa Serikali ipate ridhaa ya mahakama katika kufanya maamuzi yoyote ya kuliadhibu gazeti kwa kutoa taarifa zenye  maudhui yasiofaa kwa asilimia 54.Japokuwa wananchi wana mtazamo thabiti kuhusu upatikanaji wa taarifa na uhuru wa kuzungumza, ni wananchi wachache sana wanaofahamu sheria zinazohusiana na masuala ya habari,"amesema. 

Kuhusu Sheria inayofahamika zaidi katika suala hilo ni Sheria ya Makosa ya Mtandao (2015), ambayo inafahamika na asilimia 10 ya wananchi huku asilimia 4 pekee ya wananchi wakifahamu Sheria ya Huduma za Habari (2016). 

Pia wananchi wengi pia hawajaunganishwa kwenye mifumo ya uraia ambapo ni mwananchi 1 kati ya 4 au pungufu mwenye cheti cha kuzaliwa asilimia 25, kitambulisho cha uraia asilimia 21, leseni ya udereva asilimia 9 na hati ya kusafiria asilimia 5. Hata hivyo, karibu wananchi wote asilimia 98 wana vitambulisho vya mpiga kura

Eyakuze, anamesema wananchi wanaunga mkono kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa taarifa na uhuru wa kujieleza lakini ukweli wa mambo ni kwamba hawaombi taarifa hizo, wana imani duni na vyanzo vyote vya taarifa ukiweka kando kauli zinazotolewa na Rais na Waziri Mkuu, na hawajioni kama wanaweza kuwakosoa viongozi wakuu wa serikali.

 “Kutokana na kwamba hivi karibuni serikali imepitisha kanuni za Sheria ya Upatikanaji wa Taarifa tuna imani kuwa itakidhi kiu ya wananchi ya kupata taarifa kutoka serikalini. 

"Tunaishauri Serikali kuweka wazi taarifa ili kuyafikia matarajio ya wananchi. Cha kusikitisha, wananchi wanakamatwa na serikari kwa kujieleza kupitia mitandao ya kijamii. Ni vyema serikali ikatambua thamani ya mijadala huru ya umma na ukosoaji wenye lengo la kujenga katika mapambano dhidi ya rushwa na katika harakati za kuelekea kuwa nchi ya uchumi wa kati,"amesema.

Akifafanua kuhusu utafiti huo amesema uwakilishi wa Tanzania Bara pekee, Zanzibar haihusiki  na kwa  maelezo zaidi kuhusu mbinu za utafiti huu kwa anayetaka kujua zaidi atembelee www.twaweza.org/sauti. Takwimu za muhtasari huo zilikusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,519 kutoka awamu ya 25 ya kundi la pili la Sauti za Wananchi, na zilikusanywa kati ya Novemba 7 na Novemba 27 mwaka 2017.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...