Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega, amesema kuwa siku za wanaoagiza nyama, maziwa na samaki kutoka nje ya nchi, zinahesabika kutokana na nchi kuwa na mifigo ya kutosha kama vile Ngombe, Mbuzi, Kondoo, Kuku na Punda na hivyo Taifa kama Tanzania halina sababu yoyote ya kuagiza mazao hayo ya mifugo na uvuvi kutoka nje ya nchi.

Naibu waziri Ulega aliyasema hayo alipokuwa katika ziara ya siku tatu Mkoani Kigoma ya kutembelea Mwalo wa Samaki wa Muyobozi Uliyopo Wilayani Uvinza,Mwalo wa Kibirizi na kituo cha Taasisi ya Tafiti za Uvuvi Tanzania TAFIRI Kigoma.

“Sioni kwanini tuagize nyama na maziwa toka nje ya nchi, hatuwezi kuendelea kuangiza nyama, maziwa na hata mazao ya uvuvi, kwa nini tusiwekeze katika rasilimali zetu za ndani katika mifugo na samaki na kuongeza pato la taifa? “Aliuliza Ulega.

Ulega aliongeza kwa kusema kuwa Wizara yake haitawavumilia waafanyabiashara wanaoagiza nyama, maziwa na mazao ya samaki toka nje ya nchi kwani sekya ya mifugo na uvuvi ni sekta ambazo zikitumika vizuri zinaweza kuleta tija katika taifa.

Tarkibani “tani elfu 20 za samaki zinaingizwa kutoka nje ya nchi kila mwaka, samaki ambao wanafugwa katika maeneo mengine duniani, lakini sisi hapa nchini tunao katika mazingira ya asili.” Alisema.
Aliyesimama ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega, akiongea na watumishi wa kituo cha Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Kigoma, pamoja na watafiti hawapo pichani, alipotembelea kituo hicho, kulia ni Dkt Emmanuel Sweke, Kaimu Mkurugenzi wa kituo hicho, na kushoto ni Mkurugenzi wa tafiti na mafunzo katika chuo cha mafunzo ya uvuvi FETA Kigoma, Bw. Simtie Ambakisye, Naibu Waziri Ulega alifanya ziara katika kituo cha TAFIRI Kigoma pamoja na kutembelea mialo ya Muyobozi na Kibiri.
Kulia Dkt. Emmanuel Sweke Kaimu Mkurugenzi wa kituo wa kituo cha Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Kigoma, akimueleza jambo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega aliyekaa katikati wakiwa katika boat wakielekea kuangalia kizimba cha kufugia samaki katika maji ya ziwa Tanganyika, kushoto ni Afisa Mifugo wa Mkoa wa Kigoma Bw. Noel Byamungu.
Kushoto Dkt. Emmanuel Sweke, Kaimu Mkurugenzi wa kituo cha Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Kigoma akimuonyesha Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega katikati, kizimba cha kufugia samaki kilichopo katika maji ya ziwa Tanganyika hakipo pichani, alipotembelea kituo hicho mjini kigoma jana. Kulia ni Afisa Mifugo wa Mkoa Bw. Noel Byamungu.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...