Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa MSD, Neema Mwela, akimkabidhi Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Amaani Malima,  Mfuko wenye vifaa vya kujifungulia akina mama (Delivery Pack)
  Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa MSD, Neema Mwela, akimkabidhi msaada wa vyakula na vitu vingine Kaimu Ofisa Mfawidhi wa Makao hayo, Happyness Nyange. Kulia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa MSD, Neema Mosha.
Picha ya pamoja.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

Na Dotto Mwaibale
WANAWAKE Wafanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD), katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani wametoa msaada wa vifaa vya kujifungulia katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke pamoja na chakula kwa watoto wanaolelewa Makao ya Taifa Kurasini ya Watoto Yatima na Wenye Shida jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa MSD,  Neema Mwela alisema kwao ni faraja kubwa kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani kwa kuwatembelea wanawake wenzao katika hospitali hiyo pamoja na watoto hao.

"Sisi wanawake wa MSD tuliona ni vizuri tukasherehekea siku yetu pamoja na wakina mama waliopo katika hospitali hii pamoja na watoto wanaolelewa katika makao ya taifa ya Kurasini kwa ajili kula nao chakula cha mchana pamoja na kuwapa msaada wa chakula na vitu mbalimbali" alisema Mwela.

Mwela alisema katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke waliweza kutoa Mfuko wenye vifaa vya kujifungulia akina mama (Delivery Pack) ambao umepunguzwa bei kutoka shilingi 40,000 mpaka shilinhi 21,000 na vifaa vingine vinavyohitajika kama sabuni na miswaki.

Akizungumzia watoto Yatima na wenye shida wanaolelewa katika makao ya Kurasini alisema ni jukumu la kila mmoja wetu kuwasaidia watoto hao badala ya kuiachia serikali pekee.

Alisema kazi ya malezi ya watoto hao ni kubwa mno hivyo kila mtu anapaswa kuwa na majukumu ya kuwalea kwani kumlea mtoto tangu akiwa mdogo hadi kufikia miaka 18 ni kazi kubwa.

Kaimu Ofisa Mfawidhi wa Makao hayo, Happyness Nyange alisema katika makao hayo kuna watoto wanaosoma shule mbalimbali za msingi, sekondari na shule za awali na kuwa kama kuna mtu anayehitaji kumchukua mtoto wa kwenda kuishi naye taratibu zote zinaanzia ofisi za ustawi wa jamii zilizopo kwenye manispaa husika.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa MSD, Neema Mosha alisema waliguswa sherehe za siku ya wanawake duniani mwaka huu kuwatembelea wanawake wenzao waliopo wodi ya wazazi kwa ajili ya kujifungua pamoja na kula chakula na watoto Yatima na wale wenye shida waliopo Kurasini na kuwapa msaada wa vyakula na vifaa mbalimbali vya matumizi ya shule.

Alisema fedha za kununulia mahitaji hayo zilichangwa na wao pamoja na wafanyakazi wanaume wa MSD na kuwa thamani ya fedha kwa ajili ya kununulia vitu hivyo ilikuwa ni shilingi milioni 3.5 wakati vifaa vya hospitalini viligharimu shilingi milioni 7.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Amaani Malima alishukuru kwa msaada huo nakuleza kuwa changamoto kubwa walionayo ni majengo ya hospitali hiyo kuwa machache kutokana na ongezeko la wagonjwa na uboreshaji wa miundombinu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...