Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii
WANAFUNZI wa kike 110 waliotekwa February 19 katika shule ya bweni Dapchi nchini Nigeria wamerejeshwa nyumbani kutoka kwenye mikono ya waasi.
Waziri wa habari nchini humo Alhaj Lai Mohammed ameeleza kuwa wanafunzi 101 kati ya 110 wamerejeshwa salama na hiyo ni baada ya jeshi kuweka juhudi ili kunusuru maisha ya watoto hao.
Licha ya Wizara kutothibitisha inasemekana wasichana watano wamefariki dunia na hiyo ni kutokana na maeleza ya Aisha Kachalla Bukar (14) mmoja wa manusura hao aliyoyatoa kwa baba yake.
Pia inasadikika kuwa mmoja wa wanafunzi hao(mkristo) bado anaendelea kushikiliwa na waasi hao baada ya kukataa kuslimu.Rais wa nchi hiyo Muhammadu Buhari ameeleza kuwa janga la utekaji ni la kitaifa na ametoa pole kwa waathirika wote.
Ifahamike kuwa mwaka 2014 wanafunzi 300 walitekwa huko Chibok na hadi sasa wanafunzi 100 bado hawajapatikana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...