Na Woinde Shizza-Arusha.

WAZAZI na walezi nchini wametakiwa kutimiza wajibu wao wa kuwalea watoto kwa kufuata maadili ya Mtanzania na kuacha kuiga tamaduni za kigeni.

Imefafanuliwa kuna baadhi ya tamaduni za kigeni wanazoziiga zinachangia kusababisha mporomoko wa maadili katika jamii zetu .Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Tanzania Gara Godfrey Mheluka wakati akifunga kongomano la kujadili maadili mema na uzalendo kwa ajili ya ustawi wa Arusha yao na Taifa kwa ujumla.

Kongamano hilo lililoandaliwa na Jumuiya ya Wazazi ya CCM Mkoa Arusha na lilishirikisha wananchi ,viongozi wa dini ,vyombo vya usalama pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali na sekta binafsi iliyofanyikia katika ukumbi wa Triple A jijini hapa.

Mheluka amesema wazazi wengi wamekuwa wanalea watoto kwa kufuata tamaduni za wenzetu wa nchi za nje wakidai kuwa ndio malezi bora kwa watoto na ya kisasa kitu ambacho si kizuri kwani baadhi ya tamaduni za  wenzetu ukiangalia za kutoka nchi za kimagharibi zinaporomosho maadili kwa watoto wetu.

“Ukithamini tamaduni za kimagharibi na ukaacha za kwetu na ukamuacha mtoto nae akathamini tamaduni hizo hizo ujue umempoteza mtoto na umemuaribu kabisa.Unakuta mzazi anaona mtoto anavaa mlegezo au kimini badala ya kumkataza anamuacha anaona kuwa wake ndio mjanja.

"Huo si ujanja ni ujinga na ni kumuaribu mtoto unatakiwa umwambie mtoto hivi sio vyema.Nikiwauliza wazazi hivi nyie mngelelewa hivyo au mngelelewa vibaya je leo mngekuwepo hapo mlipo?Ni wajibu wetu kuwalea watoto wetu kwa kufuata utamaduni wetu mzuri wenye maadili ili kuandaa viongozi wazuri wa baada na wazazi wazuri wa baadae “amesema Mheluka.
Naibu Katibu Mkuu Wazazi CCM Tanzania bara Godfrey Mheluka akiwahutubia wananchi waliohudhuria kongamano la kujadili 'aadili mema na uzalendo ni ustawi wa Arusha yetu na Taifa letu kwa ujumla ,kongamano lililoandaliwa na Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Arusha.
Baadhi ya viongozi  mbalimbali meza kuu wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye kongamano hilo. 
Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi CCM mkoa wa Arusha Dkt John Palanjo akizungumza na wananchi waliohudhuria katika kongamano hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...