Na Ripota Wetu,Globu ya Kjamii

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewasihi viongozi wa dini nchini wasitumie mahubiri yao kuharibu amani au kuleta mgongano katika jamii.

Pia amesema Serikali inatambua wako watu wanaotaka kuharibu amani iliyopo nchini na ametaka watu hao wasipewe nafasi.

Akizungumza katika mkutano mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) uliofanyika Dodoma,Majaliwa amewasihi viongozi wa dini,mahubiri yao yasiwe chanzo cha uvunjifu wa amani na kufafanua Serikali haitasita kuchukua hatua licha ya kwamba inawajali,kuwathamini na kuwaheshimu viongozi wa dini.

Ameeleza kamwe nyumba za ibada zisiwe kiwanda cha kuzalisha chuki.Kuhusu watu wanaotaka kuharibu amani ya nchi,amefafanua Serikali inatambua wapo watu wa aina hiyo.

"Nawaomba viongozi wa dini kutumia Msahafu na Biblia kuhubiri amani," amesisitiza.Kwa upande wa  Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tamisemi Suleiman Jaffo amewaomba viongozi wa dini waendelee kusimamia maadili na amani iliyopo nchini.

Awali Muft sheikh Abubakar Zubeir amesema Bakwata inaendelea na kazi ya kuwaunganisha Waislam wa madhehebu yote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...