WAZIRI
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba anatarajiwa kuwa mgeni
rasmi katika Tamasha la Pasaka linalotarajia kufanyika Aprili Mosi mwaka
huu katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Kamati
ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Alex Msama amesema kuwa Nchemba
amethibitisha kuwa mgeni rasmi kwenye tamasha hilo.
Msama
ameongeza kuwa awali mgeni rasmi alikuwa awe Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mama Samiah Suluhu lakini imeshindikana
kutokana na kukabiliwa na majukumu mengine ya kikazi na hivyo Waziri
Mwigulu atamwakilisha katika uzinduzi wa tamasha hilo.
Mbali
na Mwigulu, viongozi wengine wanaotarajiwa kuhudhuria hafla hiyo ni
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi, Angelina Mabula,
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella na Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Mwanza, DCP Ahmed Msangi.
Aidha,
Msama amesema kwamba katika tamasha hilo kunatarajiwa kuwakutanisha
zaidi ya waimbaji wa kitaifa na kimataifa na akawataja baadhi ya
waimbaji ambao tayari wamethibitisha kuhudhuria kuwa ni, Rose Mhando,
ambaye atazindua albamu yake mpya ya ‘Usivunjike Moyo’, Angel Benard,
Bonny Mwaitege, Jesca Honore, Christina Shusho, Christopher Muhangila,
Upendo Nkone na wengine kibao.
“Niwaambie
ndugu waandishi wa habari, maandalizi yanaenda vizuri kwani tumejipanga
vyema kuhakikisha wananchi watakaofika siku hiyo wanapata burudani ya
kutosha na kulishwa neno la Mungu kupitia ujumbe wa nyimbo za waimbaji
na ulinzi wa kutosha utakuwepo kwani tayari jeshi la polisi litakuwepo
kuhakikisha amani na utulivu upo na hivyo nawaomba wakazi wa maeneo hayo
wajitokeze kwa wingi,” amesema.
Amebainisha
kuwa viingilio siku hiyo kwa wakazi wa Mwanza na maeneo mengine
yanayozunguka eneo hilo kwamba vitakuwa ni Shilingi 5,000 kwa wakubwa na
shilingi 2,000, kwa watoto huku kwa Mkoa wa Simiyu Aprili 2 mwaka huu,
wakubwa wataingia kwa shilingi 3,000 na watoto 2,000.
Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama akitoa ufafanuzi juu ya ujio wa mgeni rsmi ambaye ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu ambaye atawakilishwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Mwigulu Nchemba. Kushoto ni Mratibu wa Tamasha hilo, Jimmy Charles (kushoto).
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mwandaaji wa tamasha la Pasaka kanda ya Ziwa,Alex Msama alipokuwa akielezea kukamilika kwa maandalizi ya tamasha hilo sambamba na mambo mbengine mbalimbali
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...