Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji Nchini, imeamua kuzikutanisha wizara saba zinazohusika moja kwa moja na changamoto zinazopunguza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wafanyabiashara na Wawekezaji mpakani mwa Tanzania na Zambia.

Akiongea wakati wa ziara ya kutembelea maeneo ya utekelezaji wa Mpango wa maboresho ya Mazingira ya biashara na uwekezaji katika mkoa wa Songwe na maeneo yaliyopo mpakani mwa Tanzania na Zambia, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa, Faustin Kamuzora amesema mara baada ya kuhitimisha ziara yake tarehe 17 Machi, 2018, atakutana na makatibu wakuu wa wizara zinazopaswa kutoa suluhisho la changamoto hizo.

“Nitakutana na makatibu wakuu wenzangu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Mambo ya nje na Ushrikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Ofisi ya Rais-Tawala za mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) na naamini maazimio tutakayotoa katika kikao hicho yatakuwa suluhisho la kuondoa changamoto zinazojitokeza hapa mpakani mwa Tanzania na Zambia” , amesema Kamuzora.

Akibainisha changamoto za mazingira ya Biashara na uwekezaji mpakani mwa Tanzania na Zambia, Mkuu wa mkoa wa Songwe, Luteni Mstaafu, Chiku Galawa amesema, changamoto kubwa mpakani hapo ni usalama kwa wafanyabiashara na biashara zao, ambapo kwa mazingira ya mpaka huo imekuwa vigumu kuuimarisha.
Mkuu wa mkoa wa Songwe, Luteni Mstaafu, Chiku Galawa akiteta jambo na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa, Faustin Kamuzora wakati wa ziara ya kutembelea maeneo ya utekelezaji wa Mpango wa maboresho ya Mazingira ya biashara na uwekezaji mkoani Songwe, tarehe 17 Machi, 2018.


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa, Faustin Kamuzora akiendesha kikao kilicho jumuisha watendaji wa serikali na sekta binafsi wakati wa ziara ya kutembelea maeneo ya utekelezaji wa Mpango wa maboresho ya Mazingira ya biashara na uwekezaji mkoani Songwe, tarehe 17 Machi, 2018.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa, Faustin Kamuzora akiongozwa na Meneja wa Kituo cha Forodha cha Pamoja Tunduma, Jomimosa Nsindo wakati wa ziara ya kutembelea maeneo ya utekelezaji wa maboresho ya Mazingira ya biashara na uwekezaji , mpakani mwa Tanzania na Zambia, tarehe 17 Machi, 2018.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa, Faustin Kamuzora akifuatilia maelezo ya wateja wa Kituo cha Forodha cha Pamoja Tunduma (hawapo pichani) wakati wa ziara ya kutembelea maeneo ya utekelezaji wa maboresho ya Mazingira ya biashara na uwekezaji , mpakani mwa Tanzania na Zambia, tarehe 17 Machi, 2018. PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...