Na Said Mwishehe,Globu  ya jamii

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema kuwa kumebainika uwepo wa virusi vya homa ya Dangue nchini huku ikiwata hofu wananchi na tayari imeanza kuchukua hutua mbalimbali kukabiliana nao.

Akitoa tamko la Serikali kuhusu uwepo wa ugonjwa hu, Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kutokana na vipimo vilivyofanya katika maabara ya Taifa International kupelekewa sampuli za wagonjwa kutoka katika Hospitali ya Intarnetional School of Tanganyika (IST)ya Dar es Salaam, waliohisiwa kuwa na ugonjwa wa malaria lakini vipimo vyao havikubaini uwepo wa ugonjwa huo.

Amefafanua kipindi cha kati ya Januari 2018 hadi sasa kati ya sampuli 13 zilizopokelewa kutoka IST 11 zilionesha uwepo wa virusi vya dangue na kuongeza ikumbukwe hiyo si mara ya kwanza kwa ugonjwa huo kuripotiwa hapa nchini kwani ulishawahi kuripotiwa miaka ya 2010,2013 na mwaka 2014.

"Taarifa ya uwepo wa homa hiyo ya Dangue si ya kushangaza kwani mbu anayeeneza virusi vya ugonjwa huu bado yupo katika mazingira yetu.Homa ya Dangue ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinavyoenezwa na mbu wa aina ya Aedes ambao ni weusi na wenye madoa meupe yenye kung'aa,"amesema Waziri Mwalimu.

Kuhusu dalili za ugonjwa huo, amesema ni homa ya ghafla, kuumwa kichwa hasa sehemu za macho, maumivu ya viungo na uchuvu.Dalili hizo huanza kujitokeza kati ya siku 3 hadi 14 tangu mtu alipoambukizwa virusi vya homa ya Dangue.

Mwalimu amesema wakati mwingine dalili za ugonjwa huo zinaweza kufanana sana na dalili za Malaria,hivyo basi wananchi wahakikishe wakipata homa wapime ili kugundua kama wana vimelea vya malaria au dangue au sababu nyingine ili hatua stahiki zichukuliwe.

Pia amesema ni mara chache mgonjwa anaweza kutokwa na damu sehemu za fizi mdomoni, puani kwenye macho na pia kwenye njia ya haja kubwa au ndogo.Mbu wanao eneza homa ya dangue hupendelea kuzaliana kwenye maji yaliyotuama karibu na makazi ya watu, ndani ya nyumba na viluilui vya mbu hao huweza kuishi katika mazingira ya ndani ya nyumba mpaka wakawa mbu kamili na kuanza kusambaza ugonjwa huu kwa binadamu.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...