Zanzibar inaweza kuimarika zaidi kiuchumi, Maendeleo na Ustawi wa Jamii endapo uwekezaji katika Sekta ya Utalii, ujenzi wa Miji Mipya ya Nyumba za Makaazi ya Wananchi wa kawaida, Uvuvi, pamoja na Mifugo itajengewa miundombinu imara katika utekelezaji wake.

Hayo yamejiri kufuatia Kikao cha pamoja kati ya Ujumbe wa Wawekezaji Wanane kutoka Nchini Misri ukiongozwa na Bwana Amgad Hassoun ulipozungumza na Ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ukiongoza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo Vuga Mjini Zanzibar.

Mmoja wa Viongozi wa Ujumbe huo kutoka Misri Profesa Hossam El – Borombaly alisema zipo Taasisi na Makampuni ya Uwekezaji Nchini Misri yenye uwezo wa kuwekeza katika Sekta za Uvuvi, Miji Mipya, Mifugo na Miradi ya Utalii lakini kinachohitajika ni namna ya kuitekeleza kupitia Mikopo ya Benki zilizojitolea kusimamia Miradi hiyo.

Profesa Hossam alisema ujenzi wa Miji ya Kisasa ambayo Misri imeshakuwa na uzoefu mkubwa inaweza kustawisha Wananchi wa Kipato cha chini kwa kupata Makaazi bora sambamba na upatikanaji wa Ofisi zenye hadhi inayokubalika Kimataifa.

Alieleza kwamba mradi huo unazingatia hali halisi ya Kimazingira hasa ikitiliwa maanani mfumo wa misimu ya hali ya hewa kama ule wa masika wakati mwengine huambatana na mvua kubwa zinazosababisha mafuriko na kuleta Maafa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kushoto akizungumza na Ujumbe wa Viongozi Wanane wa Taasisi za Uwekezaji kutoka Nchini Misri hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Kiongozi wa Ujumbe wa Viongozi Wanane wa Taasisi za Uwekezaji kutoka Nchini Misri Bwana Amgad Hassoun wa Pili kutoka Kulia akimueleza Balozi Seif maeneo ambayo Kampuni za Misri zinaweza kuwekeza Miradi yao Visiwani Zanzibar. Picha na – OMPR – ZNZ.

 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...