Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na Taasisi za Kiraia katika kuona malengo na dhamira zilizojipangia katika kuwahudumia Wananchi zinafanikiwa vyema.

Alisema Taasisi nyingi za Kiraia zilizoanzishwa Nchini zimeonyesha mwanga wa matumaini katika kusaidia huduma za Kijamii hasa kwenye Sekta na miradi ya Elimu jambo ambalo Serikali inastahiki kujivunia na kuendelea kuzipa ushirikiano huo.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Uongozi wa Taasisi ya Kiraia ya kumjengea uwezo wa Kielimu Mtoto wa Kike na Mwanamke ya Forum for African women Educationalist {FAWE} hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.

Alisema kundi kubwa la Wanawake hivi sasa tayari limeshaamka katika kufukuzia maendeleo hasa katika masuala ya Kielimu kupitia Taasisi za Kiraia jambo ambalo limewapa nafasi ya kushiriki katika makundi mbali mbali ya maamuzi katika maeneo yao.

“ Kazi kubwa iliyofanywa na FAWE imewezesha kutoa msukumo kwa kundi kubwa la wanawake kuamka katika kufukuzia maendeleo”. Alisema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Alieleza kwamba Historia inaonyesha wazi jinsi gani Mwanamke alivyokuwa akikosa fursa kwa Karne nyingi zilizopita kutokana na mfumo dume uliokuwa ukitumika kuwanyima haki zao hasa katika fursa za Uongozi na Maamuzi ya msingi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kati kati akizungumza na Uongozi wa Taasisi ya Kiraia ya kumjengea uwezo wa Kielimu Mtoto wa Kike na Mwanamke ya Forum for African women Educationalist {FAWE} hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Wa kwanza kutoka kushoto ni Mratibu wa FAWE Bibi Hinda Abdullah Ajmin na wa kwanza kutoka Kulia ni Mshika Fedha wa FAWE Bibi Sabra Issa Mohammed.
Mratibu wa Fawe Bibi Hinda Abdullah Ajmin Kushoto akimfafanulia Balozi Seif Miradi mbali mbali iliyoanzishwa na Taasisi hiyo ambayo tayari imeshamsaidia Mtoto wa Kike kujikomboa Kielimu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alizungumza na Viongozi wa Dini pamoja na wa Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto kujadiliana Wimbi la vitendo vya udhalilishaji wa Kijinsia na kuangalia Mikakati ya kupambana na janga hilo. Picha na – OMPR – ZNZ.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...