Na Agness Francis,Blogu ya Jamii

BARAZA  la sanaa Taifa (BASATA) lenye dhamana ya kufufua kukuza na kuendesha sekta ya sanaa   kutoa tuzo kwa wanafunzi wa kidato cha 4 kwa shule 5 za Sekondari waliofanya vizuri masoma ya sanaa  hapa nchini.

Shule hizo zitakazo husika  katika kupewa tuzo hizo ni Mbeya Sekondari wanafunzi 2,Dodoma Sekondari 1,Edmund-Recesinon Sekondari Arusha 1,Mvuha Sekondari Morogoro 1 pamoja na Murungwa sekondari Kagera 2.

Baraza hilo limeamua kufufua  programu  endelevu ya utoaji wa tuzo kwa wanafunzi  wa shule za sekondari waliofanya vizuri katika mitihani ya kidato cha 4 kwa mujibu wa sheria namba 23 mwaka 1984.

Ambapo safari hii watatoa kwa wanafunzi waliomaliza mwaka 2016 na kufaulu katika masomo ya sanaa za ufundi,maonyesho na muziki. 

Aidha amezungumza na wandishi wa habari  katika ofisi zake basata Jijini Dar Es Salaam mkurugenzi wa masoko na ukuzaji sanaa Basata Vivian Shalua  amesema kuwa utoaji wa tuzo hizo itachochea wanafunzi wengi kusoma masomo hayo katika kazi za sanaa na kuwasaidia kuongeza ufaulu wao darasani hasa ukizingatia sanaa ni nyenzo katika kumuandaa mtoto kielimu na kimaadili.

"Sanaa ni chanzo cha ajira kwa vijana wengi ambao wameweza kijipa kipato na umaarufu kupitia fani hizi za Sanaa,hata hivyo masomo haya yamekuwa hayapatiwi kipaumbele kama yalivyo masomo mengine katika shule za msingi na sekondari"amesema Mama Shalua.

Mama shalua ametoa wito kwa kuwaalika  wadau wote wa sanaa  hapa nchini kufika kushuhudia utoaji wa tuzo hizo ambazo kauli mbiu yake (sanaa ni kazi ,nchi yangu kwanza).

Tuzo hizo zitatolewa Aprili 28 mwaka huu saa 4 asubui katika ukumbi wa Basata Sharifushamba Ilala Jijini Dar Es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...