Hospitali na kliniki nyingi nchini zina tatizo la ukosefu wa dawa, vifaa na vitanda hasa katika hospitali za rufaa. Katika kukabiliana na uhaba huu unaosumbua taifa, benki ya Exim Tanzania, yenye uwepo wa kimataifa imeanzisha mradi unaolenga kusaidia upungufu wa vitanda katika wodi za wazazi kwenye hospitali nchini - hivyo benki ya Exim itatoa magodoro and vitanda 500 katika hospitali za serikali katika mikoa 13 nchini kama sehemu ya kampeni yake ya mwaka yenye lengo la kusherehekea miaka 20 ya kutumikia jamii.
Benki ya Exim Tanzania imekabidhi vitanda na magodoro 40 kwa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro, jijini Morogoro. Benki ya Exim Tanzania iliadhimisha miaka 20 ya huduma, mwezi wa Agosti mwaka jana, kwa kuzindua mradi wa mwaka mzima unaoitwa “miaka 20 ya kujali jamii” ambao Benki hiyo itawekeza katika sekta ya afya Tanzania hasa kwenye kuboresha huduma za afya zinazotolewa kwa wakina mama na wanawake. 
Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro ni hospitali ya tisa kupokea mchango huu, baada ya hospitali ya rufaa ya Mwananyamala mwezi uliopita, hospitali  ya rufaa ya Bombo, mkoani Tanga mwezi Febuari, hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mbeya mwezi Januari, hospitali ya Mount Meru, Arusha mwezi Desemba, Hospital ya rufaa Dodoma mwezi Novemba, hospitali ya rufaa Ligula, Mtwara mwezi Oktoba, Hospitali ya Mnazi Mmoja, Unguja, Zanzibar mwezi Septemba na Hospitali ya rufaa Temeke, Dar es Salaam mwezi wa nane mwaka jana.
Mkuu wa idara ya masoko wa benki ya Exim Tanzania, Stanley Kafu  akizungumza wakati wa makabidhiano ya vitanda na magodoro 40 katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kupitia kampeni yao ya maadhimisho ya miaka 20 ya kujali jamii kwa benki hiyo.
Mwenyekiti wa bodi ya hospitali ya rufaa ya Morogoro, Dk Lucy Nkya akipokea Vitanda na magodoro 40 kutoka kwa Mkuu wa idara ya masoko wa benki ya Exim Tanzania, Stanley Kafu, yaliyotolewa na benki ya Exim kupitia kampeni yao ya maadhimisho ya miaka 20 ya benki hiyo yenye kauli mbiu ya "miaka 20 ya kujali jamii".
Mganga mkuu mkoa wa Morogoro, Dk Francis Jacob akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi vitanda na mahodoro 40 kutoka benki ya Exim Tanzania kupitia kampeni yao ya maadhimisho ya miaka 20 ya kujali jamii kwa benki hiyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...