THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

DC MJEMA AONJA ADHA YA MAFURIKO AKIKAGUA MIUNDOMBINU ILALA

 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akisaidiwa kuvuka kwenye daraja la muda alipokuwa akikagua leo daraja la Mto Msimbazi linalounganisha Ulongoni B na Gongo la Mboto, Dar es Salaam, ambalo ni moja ya madaraja yaliyobomoka kutokana athari za mvua za masika zinazoendelea kunyesha. Mjema alifanya ziara ya kukagua miundombinu ya barabara iliyoathiriwa na mvua katika wilaya hiyo. PICHA NA RICHARD MWAIKENDA, KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mkuu wa Wilaya Mjema, akizungumza na wakazi wa Ulongoni baada ya kuwafuata upande wa pili kwa kutumia daraja hilo hatari.

 Mjema akiondoka baada ya kukagua daraja hilo la Ulongoni B.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mjema (kulia) akishauriana na Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Edward Mpogolo pamoja na Mkurugenzi wa Manisapaa ya wilaya hiyo, Msongela Palela alipofika kukagua daraja la Banguo Pugu Mnadani eneo ambalo mto umeacha kupita darajani na kumega eneo la barabara hali iliyosababisha kukata mawasiliano ya usafiri katika eneo hilo.
 Wakiangalia jinsi mto Msimbazi ulivyoacha mkondo wake wa kawaida na kumega ardhi maeneo ya makazi ya watu pamoja na kuharibu barabara.
 Baadhi ya nyumba eneo la Bangua ambazo zimo hatarini kubomolewa na mafuriko.