Na Verdiana Mgoma, Msaidizi wa Mbunge

WASOMI na wananchi wapenda maendeleo waishio nje na ndani ya Kijiji cha Butata wameungana pamoja ili kufanikisha ujenzi wa zahanati katika kijiji chao ili kuondoa adha kubwa ya ukosefu wa huduma za kiafaya kijijini hapo.

Awali akizungumza na Msaidizi wa Mbunge ambae ni mwandishi wa habari hizi, Mwenyekiti wa Kijiji cha Butata Ndugu Cleophace M. Kasala ameeleza kuwa Wananchi wa Kijiji cha Butata wamekuwa na muamko katika suala la ujenzi wa zahanati hata kufikia hatua ya kuhamasishana kwa kuchangia nguvu kazi ili kuwaunga mkono ndugu zao waliojitolea kuwachangia mifuko ya saruji na fedha za kujengea zahanati hiyo.

"Wananchi baada ya kupata Wafadhili ambao ni Wazawa wa Kijiji cha Butata wao wamehamasika na kujitolea kuchimba msingi, kusomba mawe, mchanga n.k"

Kwa upande wake Amina Kasaka ambaye pia ni mkazi wa Kijiji cha Butata ameeleza kuwa, wao kama akina mama kwa kipindi kirefu wamekuwa wakitembea umbali mrefu kufuata huduma ya afya hali ambayo imekuwa ikiwapa wakati mgumu sana katika upatikanaji wa huduma za afya. Ameongezea kuwa hali hiyo imekuwa ikihatarisha maisha ya mama na mtoto na hata wazee.

Naye Diwani wa Kata ya Bukima Mh. January Simula ameeleza mpango kazi wa Kata yake katika ujenzi wa zahanati kwa kila kijiji. Katika kutekeleza Ilani ya CCM, wamefanikisha kwa vijiji viwili ambapo hadi sasa wana zahanati moja ya Bukima na ya pili wameanza ujenzi wake Kijijini Butata. Pia Serikali ya Kata hiyo imeanza hatua za upanuzi wa Zahanati ya Bukima kuwa Kituo cha Afya cha Kata.

Katika kulifanikisha hilo, Diwani amesema yuko bega kwa bega na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Prof. S. Muhongo kwa hamasa na michango yake kwenye sekta za Afya, Elimu na Kilimo ikiwa ni vipaumbele vya Jimbo la Musoma Vijijini.

Ofisi ya Mbunge imesema inashirikiana na wananchi wapenda maendeleo wa Kijiji cha Butata kufanikisha ujenzi wa zahanati hiyo.

Picha ya hapo chini inaonyesha ujenzi wa Zahanati ya Butata ikiwa kwenye hatua ya ujenzi wa msingi.

Ofisi ya Mbunge
www.musomavijijini.or.tz

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...