Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru jitaifa charles Kabeho ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma, kwa kuzingatia na kujenga majengo yenye ubora kwa kutumia gharama nafuu.

Hivyo amezishauri Halmashauri zingine kuiga mfano huo ambapo amesema hayo wakati akikagua mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa vinne na ofisi mbili katika Shule ya Msingi Kishanga, vilivyo gharimu zaidi ya Sh. milioni 100 pamoja na ujenzi wa Kituo cha Afya na Nyumba ya mganga Janda kilicho gharimu kiasi cha Sh. milioni 400, ikiwa ni fedha ya ndani.

Kiongozi huyo wakati akizindua na kuweka jiwe la msingi jana amesema amefurahishwa na viongozi wa Halmashauri hiyo kwa ubunifu walioufanya na uzalendo baada ya kupatiwa fedha za Serikali na kuamua kujenga ujenzi usio tumia gharama kubwa ili kuwasaidia wananchi kupata huduma mapema.

Aidha Kabeho ametoa mwito kwa makandarasi waliipewa zabuni za kujenga miradi katika Halmashauri mbalimbali nchini kufanya kazi kwa kuzingatia viwango vilivyo ainishwa kwenye mikataba yao na kuhakikisha miradi wanayoijenga inakuwa ni yenye ubora .Mwito huo aliutoa wilayani wakati akikagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kusisitiza kuwa kwa sasa serikali imetoa kipaumbele kwa makandarasi wazawa kufanya Kazi ili kuharakisha maendeleo ya nchi yao hivyo wafanye Kazi vizuri.

Hata hivyo aliwaagiza wananchi kuhakikisha wanailinda na kuitunza miradi yote ya maendeleo ili vizazi vijavyo navyo viendelee kunufaika na miradi hiyo kwani serikali imejipanga kutatua kero za wananchi kwa kuwawekea huduma za kijamii karibu ikiwa ni pamoja na hospitali, vituo vya afya na Shule ili wanafunzi wapate elimu karibu na maeneo wanayoishi.Wakizungumza mara baada ya uzinduzi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Msingi Kishanga, Bernadetha Samsoni alisema, wanaipongeza Serikali ya awamu ya tano kwa kazi kubwa anayoifanya.Pia wanaiomba Serikali kuendelea kufanya miradi hiyo katika vijiji vingine ili kuondoa kero za upatikanaji huduma kwa Wananchi.

Jhoni Bhalagaye ni Mkazi wa Kijiji cha Janda amesema wanaipongeza Serikali kwa kuwajengea Kituo cha afya kwani mwanzoni walikuwa wakipata shida kupata huduma za afya katika Wilaya ya Kasulu."Lakini baada ya Kituo hicho kikikamilika tutakuwa na amani na tutapata huduma vizuri," amesema.

Kazi nyingine zilizofanywa na Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani Buhigwe ni kuweka jiwe la msingi Katika ujenzi wa Barabara ya Muzeze Kigogwe, inayotekelezwa na serikali kupitia wakala wa Barabara vijijini (TARURA )kuzindua jengo la kituo cha biashara katika kiiiji cha Buhigwe na kuzindua klabu ya wapinga rushwa katika shule ya msingi Biharu na uzinduzi wa Nyumba bora katika Kijiji cha Muyama .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...