Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

JAMII imehimizwa kupanda miti hasa ya asili ambayo ipo hatarini kutoweka pamoja na kulinda mazingira kwa faida na manufaa ya kizazi kijacho.

Aidha wananchi wameaswa kuacha kukata miti na misitu ovyo kwani kwa kufanya hivyo kunasababisha kuondoa uoto wa asili.

Rai hiyo ilitolewa na mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali la – SAHO-linalojishughulisha na masuala ya upandaji miti na kuhimiza kutunza mazingira , Emmanuel Luamba wakati wa uzinduzi wao wa kampeni ya upandaji miti kata ya Visiga ,Kibaha Mkoani Pwani.

Alisema wananchi wanahimizwa kupanda miti lakini isisahaulike miti ya asili ikiwemo mninga,mkwaju,mkongo ambayo ina faida zake katika kukuza uchumi ,kuleta hewa safi na kuwa na nchi ya kijani.

Luamba alieleza wameotesha miche ya miti ya asili ipatayo 10,000 ambayo wanaisambaza iweze kupandwa taasisi za umma ikiwemo mashuleni ,kwa wananchi kata ya Visiga, kisha ngazi ya halmashauri na baadae Mkoa.

“Tumeanzia taasisi za umma ikiwemo shule mbalimbali na jamii ili kuwa na uelewa wa kujua faida za miti hii kwa manufaa ya sasa na vizazi vinavyokuja” alielezea Luamba.Akizungumzia ujio wa shirika hilo ,mwenyekiti huyo alibainisha wanatarajia kuwa na matawi nchi nzima .
Mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na masuala ya upandaji miti la SAHO,(wa kwanza kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wenzake baada ya kupanda moja ya mche wa mti wa asili ,katika shule ya msingi Visiga wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti ya asili inayofanywa na shirika hilo
Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Kibaha, Fokas Bundala(wa kushoto) akipanda mche wa mti wa asili aina ya mninga ,katika shule ya msingi Visiga wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti ya asili inayofanywa na shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na masuala ya upandaji miti la SAHO,(wa kulia) ni diwani kata ya Visiga Mbegu Kambi Legeza.Picha na Mwamvua Mwinyi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...