Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii

IMEELEZWA watu pekee wanaoweza kumaliza migogoro ya ardhi nchini ni pande mbili ambazo zipo kwenye mgogoro na si vinginevyo na hata watalaam wanapokwenda basi ni kwa ajili ya kuweka mipaka tu.

Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Halmashaui ya Wilaya ya Morogoro, Kibena Kimu wakati wa ufunguzi wa mdahalo wa haki za ardhi wilayani Morogoro uliondaliwa na Shirika la mradi la PELUM Tanzania.

Mdahalo huo unaofanyika kwa siku mbili na kushirikisha vijiji vitano vya Mikese Lubungo, Newland na Mfumbwe vya wilayani humo ambapo Kimu amefafanua haiweze kumaliza siku bila kupata taarifa ya mgogoro wa ardhi kutoka kati ya wakulima na wafugaji au kijiji na kijiji, kuhusu mipaka.

Ambapo kila mmoja anakidai kuingiliwa na mwenzake na hata watalaamu wakienda na GPS wanakuwa na wakati mgumu kutatua mgogoro huo.

"Nimekuwa nikiwashauri wakae pande zote mbili zinazolumbana kuhusu ardhi na wanapokubaliana inakuwa rahisi kumaliza mgogoro na watalaam wa ardhi wanakuwa sehemu ya mashahidi tu,"amesema.

Ameongeza elimu inayotolewa na PELUM kuhusu kutambua rasilimali ardhi na namna gani ya kumiliki na kuwa na uwezo wa kushughulikia migogoro ya ardhi inayojitokeza imesaidia sana wananchi.

"Kwani vijiji vyote vina mabaraza ya ardhi lakini elimu waliyopata pengine haijatosheleza. Nawashukuru PELUM kwa kazi wanayofanya na elimu wanayotoa ya kusimamia matumizi bora ya ardhi kwenye halmashauri yetu ya Morogoro.

"Rasilimali pekee tuliyonayo watanzania ni ardhi kitu ambacho nchi zingine hakipo.Tumeona ujio wa watu wengi wakija kwa ajili ya kuchukua na kumiliki na kuwekeza kwenye miuondombinu ya ardhi yetu, tusipokuwa na uwezo wa kumiliki ardhi, tunaweza kuja kuwa watumwa kwenye nchi yetu,"amesema.

Amefafanua watu wanaendesha maisha yao kwa kilimo na hali ya kawaida na kusisitiza mpango unaofanywa na PELUM wa kuwapimia vipande vya ardhi wananchi wa kawaida na kuwatengenezea hati miliki za kimila ni jambo la msingi.

"Hati hizo za kimila zitawawezesha wananchi kwenda kukopa na kuenedeleza au kuwekeza kwenye maendeleo yetu na kutengeneza viwanda vidogo.

"Hata pale wanapokuwa na changamoto za mvua na bei ya mazao basi wanaweza kuyafanya kuwa mazao ghafi na kuyatunza katika ubora mpaka pale yatakaposafirishwa,"amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...